Menu
in

Kakuta yamemkuta!

Shirikisho la soka duniani FIFA limeifungia klabu ya Chelsea kufanya usajili wa mchezaji yeyote kwa muda wa mwaka mmoja kwa kitendo chao cha kumshawishi mshambuliaji chipukizi wa Ufaransa, Gael Kakuta kuvunja mkataba wake na timu ya Lens ili ajiunge nao.

FIFA imesema Chelsea haitawezi kusajili mchezaji yeyote mpya kutoka England au sehemu yoyote duniani katika misimu miwili ya usajili kuanzia Januari 2010 na Januari 2011.

Kamati ya FIFA inayoshughulikia usuluhishi imetoa uamuzi huo baada ya klabu ya Lens kulalamika kwamba Chelsea imemshawishi mshambuliaji huyo chipukizi Gael Kakuta kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ya Ufaransa ili aweze kujiunga na vigogo hao wa England.

FIFA imemtaka Kakuta na klabu ya Chelsea kuilipa klabu ya Lens dola milioni 1.12 kama fidia. Pia Chelsea inatakiwa kuilipa Lens dola 186,000 ikiwa ni ada ya mafunzo ya mchezaji Kakuta.

Kamati hiyo ya FIFA pia, imemfungia Kakuta mwenye miaka 18 raia wa Ufaransa kucheza mechi yoyote duniani kwa muda wa miezi minne.

“Kamati ya usuluhishi imegundua kwamba Kakuta alivunja mkataba aliosajili katika timu ya Lens ya Ufaransa, ambapo kamati hiyo pia iliona kuwa Chelsea ndiyo ilimshawishi mchezaji huyo kuvunja mkataba,”ilisema taarifa ya FIFA.

“Chelsea imefungiwa kusajili wachezaji wapya kitaifa au kimataifa kwa kipindi cha misimu miwili ijayo ya usajili kufuatia kuwasilishwa kwa maamuzi ya kamati ya usuluhishi,”ilisema taarifa ya FIFA.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version