Pamoja na awali kutandwa na hali ya
hofu ya usalama nchini Darfur ambako
ndipo yanafanyika michuano ya kombe la
Kagame mwaka huu hali ni shwari na
mashindano hayo yapo katika hatua ya
Fainali na tayari timu ya APR ya
Rwanda imekua ya kwanza kutinga hatua
ya fainali katika michuano hiyo.
Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi
wa michuano hiyo walivuliwa ubingwa
huo baada ya Serikali kuzikatazia timu
hizo za Tanzania Simba, Yanga na
Falcon ya Zanzibar kutokwenda katika
michuano hiyo kutoka na hali ya
usalama.
APR imekuwa ya kwanza kuingia katika
fainali baada ya kuifunga timu ya
wenyeji wa michuano hiyo Al Mereikh El
Fasher jumla ya magoli 4-3.
Ushindi wa APR unamfanya kocha wao
Andreas Spier kutimiza ndoto zake za
kuwania ubingwa huo katika fainali
zitakazofanyika Julai2 nchini humo.
Timu hizo zilimaliza muda wa kawaida
wa dakika 90 ikiwa sare ya 1-1 na
kutakiwa kuongezwa muda wa ziada wa
dakika30 ambapo APR ilimalizia karamu
ya magoli kwa kupachika magoli mengine
matatu.
Kwa ushindi huo sasa APR inasubiri
mshindi kati ya Vital O ya Burundi
dhidi ya Ryon Sports ya Rwanda katika
nusu fainali nyingine itakayopigwa leo
kwenye uwanja wa Nagwa mjini Durfur.
Kwa matokeo hayo yanaonyesha kuwa
fainali inachezwa na timu za ugenini
baada ya wenyeji wa michuano hiyo
kutolewa mapema katika michuamno hiyo
na kuwaachia wageni wakiendeleza ubabe
wa kutwaa kombe hilo kila mwaka.
Kwa upande wa Katibu mkuu wa Baraza la
vyama vya soka ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati CECAFA Nicholous
Musonye alisema licha ya klabu za
Tanzania kushindwa kushiriki lakini
michuano hiyo imefanyika vizuri na
imeonyesha msisimko mkubwa zaidi.
“Mashindano yamefanyika
vizuri,tunashukuru kila timu imevuna
ilichopanda,kutoshiriki kwa timu za
Tanzania hakujatuathiri chochote kwani
msisimko wa mashindano umeongezeka na
hata mashabiki wa nchini Sudan
wamefurahi kiwango cha timu
zilizoshiriki”alisema Musonye.
Hata hivyo Musonye alisema kuwa
hawatatoa adhabu yoyote kwa timu nza
Tanzania kushindwa kushiriki michuano
hiyo ila watawakaribisha tena mwakani
katika michuano mingine.
Michuano hiyo inataraji kufikia tamati
mapema Jumanne ijayo kwa mchezo wa
fainali.