Liverpool wamefanikiwa kumsajili beki wa Uholanzi kutoka katika klabu
ya Southmpton.
Kwa ada ya Pauni Milioni 75, ada inayomfanya kuwa beki ghali zaidi
duniani kwa sasa.
Katika ada hii timu yake ya Celtic imefanikiwa kupata gawio la 10%-15%.
Je ni kwa namna gani, Liverpool wataenda kunufaika na Virgil Van Djik?
Kwa miaka ya hivi karibuni Liverpool wamekosa beki ambaye ni mtulivu mkubwa.
Hiki ndicho kitu cha muhimu ambacho Virgil Van Djik anachoenda
kukileta ndani ya Liverpool.
Utulivu wake na uwezo wa ku “Control” mpira kwa kiasi kikubwa kitakuwa
kitu chenye msaada kwa Liverpool.
Kwa misimu kadhaa Liverpool wamekuwa wakifungwa magoli ya krosi, kona.
Je Virgil van Djik atakuwa na msaada katika mipira ya juu?
Virgil Van Djik ni mzuri sana katika mipira ya juu, hii itakuwa na
faida kubwa sana kwa Liverpool kwenye upande wa kujilinda na upande wa
kushambulia pia.
Van Djik anajua kucheza vizuri mipira ya juu, na tatizo la Liverpool
lilikuwa kuokoa mipira ya juu inayotokana na krosi pamoja na kona.
Hata upande wa kushambulia kuna faida kwa sababu kutaipa nafasi
Liverpool kupata wigo mkubwa wa kuwa na wapiga vichwa wengi pindi
wanapokuwa wamepata kona.
Pamoja na kwamba Countinho ni mzuri wa kupiga mipira iliyokufa (free
kick), je kuna faida kwa ongezeko la Virgil Van Djik ?
Van Djik amekuwa mchezaji ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga magoli ya
mipira ya adhabu ndogo hii itaongeza kitu cha ziada katika kikosi cha
Liverpool.
Ukiachana na kwamba Virgil Van Djik anauwezo mkubwa wa kupiga mipira
ya adhabu ndogo, pia anauwezo mkubwa wa kupiga pasi.
Pasi zake zina msaada mkubwa katika kuanzisha mashambulizi ya timu.
Anapiga pasi fupi na ndefu ambazo kwa kiasi kikubwa huhamisha uwanja .
Kumekuwa na usalama mdogo kipindi ambacho mchezaji wa timu pinzani
anavyobaki na beki mmoja (one against one).
Wengi wa mabeki wa kati wa Liverpool siyo wazuri kwenye ( one against one).
Lakini Virgil Van Djik ni mzuri kwenye hili eneo , ambapo ni vigumu
kukuruhusu kupita kama mko naye wawili.
Liverpool imekuwa haina aina ya wachezaji wengi ndani ya uwanja ambao
wana kariba ya uongozi.
Ina wachezaji wachache sana wenye kariba hii ya uongozi..
Virgil Van Djik anakuja kwenye kikosi ambacho kinamwihitaji kwa sababu
kikosi kilihitaji kuwa na wachezaji wengi wenye kariba ya uongozi.
Hivo Virgil Van Djik anakuja kuongeza idadi ya wachezaji viongozi
ndani ya kikosi cha Liverpool.
Pamoja na kwamba Virgil van Djik ni mtulivu akiwa kwenye eneo lake,
pia ni mtulivu katika eneo la timu ya wapinzani.
Akipata mipira katika box la wapinzani huwa anakuwa mtulivu na huwa
ana nafasi nzuri ya kufunga.