Chama cha mchezo wa netiboli nchini Tanzania (Chaneta) kimesema hakitaweza kufanya michuano ya netiboli ya Dunia ndani ya uwanja wa Taifa (Uwanja mpya )kutokana na uwanja huo kukosa kapeti ambalo lingewekwa ndani ya uwanja huo.
Katibu mkuu wa Chaneta Anna Kibira amesema upatikanaji wa kapeti la kuchezea netiboli litachukua muda wa miezi sita hivyo mpaka kapeti lipatikane tayari mashindano yatakuwa yameshafanyika.
Kibira amesema kutoka na kukosa kapeti mashindano hayo yatafanyika nje ya uwanja wa TAIFA ambapo watatengeneza magoli pamoja na sehemu ya kukaa mashabiki na timu husika.
Amesema uamuzi huo umeafikiwa baina ya Chaneta na shirikisho la mchezo wa netiboli Duniani (IFNA) ambao walifika hapa nchini kukagua sehemu ya kufanyia mashindano hayo.
Mpaka sasa nchi nane zimethibitisha kushiriki mashindabno hayo ya Dunia yaliopangwa kufanyika September mwaka huu Jijini Dar es salaama na Tanzania ndio wenyeji wa mashindano hayo.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuanda mashindano makubwa ya mchezo huo wa Netball na hivi sasa harakati za kuanda timu ya Taifa zinaendelea.