Nchini England katika ligi kuu ya soka nchi hiyo kumepita timu nyingi zenye sifa mbalimbali na ambazo ziliwahi kushika hisia za mashabiki wa soka ulimwengu mzima. Katika timu hizo kuna timu ambazo hazikuwahi kubeba mataji yoyote ya maana lakini zimewahi kuwa zinazungumziwa kiulimwengu. Mojawapo ya vilabu hivyo ni klabu ya Southhampton. Klabu hiyo ilikuwa nigumzo kwani ilikuwa inatoaga ushindani wa kimichezo pindi ilipokuwa inacheza na vilabu vikubwa na vilabu vikubwa vilikuwa vinapata wakati mgumu sana kupata matokeo dhidi ya klabu hiyo.
Klabu hiyo haikuwa inatumia gharama kubwa katika usajili kwani wachezaji wengi ambao ilikuwa inawanunua walikuwa ni wachezaji ambao waligharimu kiasi kidogo sana cha pesa kuwapata. Klabu hiyo ilisimama katika misimamo yake hiyo licha ya kwamba mitindo ya uendeshwaji wa soka la Uingereza ilibadilika kutokana na uwekezaji mkubwa sana wa kifedha ambao ulifanywa na matajiri wakubwa katika vilabu vya nchini Uingereza. Uwekezaji ulifanya vilabu vinunue wachezaji wenye majina makubwa ambayo yaliweza kushawishi kibiashara lakini klabu hiyo ilibaki kwenye msimamo wa kuendelea kununua wachezaji chipukizi tena wasio na majina makubwa na kisha kuwageuza kuwa ni wachezaji wakubwa ambapo waliwauza kwa pesa kubwa ambayo iliwafanya wapate faida. Vilabu vikubwa nchini Uingereza vilifanya mabadiliko kwa kuanza kujenga upya viwanja vyao au kufanya marekebisho makubwa katika viwanja vyao. Vilabu viliweza kuhamia katika viwanja vipya ambavyo vilikuwa vikubwa zaidi na pia vyenye uwezo wa kubeba mashabiki wengi Zaidi lakini Southampton ilibakia katika uwanja wake wa nyumbani ambao wameupa jina la St Mary’s stadium.
Klabu ya Southampton inasifika kuzalisha vipaji kadhaa vya soka ambavyo vilivuma katika soka la England. Mifano ya wachezaji hao ni kama ifuatavyo; bekinguli wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi ambaye ni Virgil Van Dijk, kiungo wa Liverpool Adam Lallan, kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Alex Oxlade Chamberlain, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Everton na timu ya taifa ya England, Theo Walcott, kiungo mshambuliaji wa klabu za Real Madrid na Tottenham Hotspurs pamoja na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale. Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Al Nasr na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane.
Klabu ya Mtibwa Sugar ni mojawapo ya vilabu nguli nchini Tanzania. Msimu huu wa mwaka wa ligi kuu soka bara klabu hiyo imeshuka daraja. Imeshuka daraja huku ikiwa imeacha simanzi kwa mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania. Klabu hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1988 ikiwa ni timu ya wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa Sugar Estates. Mwaka 1999 klabu hiyo ilifanikiwa kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.mwaka huu walitikisa soka la Tanzania kwani walikuwa mabingwa huku wakionyesha soka safi na lenye kuvutia.
Kwa mda mrefu imekuwa inatumia uwanja wake wa nyumbani unaoitwa Manungu ambao upo Turiani Morogoro. Klabu hiyo imepita mikononi mwa makocha kadhaa ambao wameifundisha klabu hiyo. klabu hiyo kwa misimu kadhaa ilifanikiwa kuleta upinzani kwa vilabu vikubwa ndani ya soka la Tanzania. klabu hiyo imewahi kubeba makombe kadhaa nchini ikiwemo kombe la mapinduzi na mengineyo.
Klabu hiyo kwa mda mrefu imekuwa inasifika kuwa ni klabu ambayo inazalisha vipaji vya wachezaji wengi ambao wanaokuwa wanafanya vizuri katika soka la tanzania. wachezaji kadhaa kama vile Abutwalib Mshery ambaye ni kipa wa Yanga, Dickson Job wa Yanga, Ladack Chasambi wa Simba na wengineo wengi ambao wanaofanya vizuri katika ligi ya soka Tanzania bara. klabu hiyo imekuwa na utaratibu mzuri wa kusaka vipaji vichanga katika soka na kuvilea na baadaaye kuvipa nafasi kucheza katika klabu yao na pindi wanapofanya vizuri huwauza wachezaji hao katika vilabu vikubwa.
Klabu hiyo anguko lake ambalo lilipelekea kushuka daraja halikuanza ndani ya siku moja bali lilianza taratibu kwa misimu kadhaa mpaka wakafikia kwenye hatua hiyo. kwa maoni yangu Mtibwa imejikuta kwenye hali hiyo kutokana na sababu kadhaa; Kwanza Mtibwa ilianza kuachana na falsafa zake. kila klabu duniani huwa ina falsafa zake kwenye soka. falsafa ya Mtibwa ilikuwa kukuza wachezaji wachanga na wapya ambao wanakuwa wanatokea katika mikoa ya jirani na Morogoro na kisha kuwachukua wachezaji hao na kuwaendeleza na kisha kuwapa nafasi. walipoanza kuwa wanasajili wakongwe ambao wana uzoefu waligi kuu ndio wakaanza kuanguka taratibu
Pili klabu hiyo ilipoteza utambulisho(identity). kwa kipindi kirefu klabu hiyo ilikuwa inafahamika kama makazi yake ni Turiani lakini ghafla ilianza kubadilisha viwanja vya nyumbani na matokeo yake ikaanza kupoteza mashabiki taratibu taratibu. iliwahi kuhamia na kutumia uwanja wa Shabiby CCM Gairo kama uwanja wake wa nyumbani na kisha ikahamia Jamhuri Morogoro na kisha ikahamia uwanja wa Uhuru na kisha ikahamia. Kuhamahama huko kuliifanya ikawa inapoteza mashabiki wa nyumbani na hivyo klabu hiyo kukosa hamasa katika mechi zake za nyumbani.
Tatu ushindani katika ligi kuu bara umeongezeka. uwekezaji ambao umefanywa na wafanyabiashara mbalimbali umefanya ligi hiyo iwe na ushindani na kila timu ina morali ya kupambana ibakie katika ligi kuu.
kushuka daraja kwa Mtibwa ni anguko ambalo kwa baadhi ya watu limewashitua lakini kiujumla ni jambo ambalo lilitarajiwa na ni fursa ya klabu hiyo kujipanga upya kiutawala na kimiundombinu ili pindi watakaporudi wawe ni klabu yenye nguvu zaidi.