Ivory Coast wamefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuwafunga Cameroon 1-0 katika mechi ya Kundi D.
Bao la Max Gradel katika dakika ya 35 lilitosha kuwavusha Ivory Coast, huku Cameroon wakishika mkia, ukiwa ni mwaka waliofanya vibaya zaidi tangu waanze kushiriki mashindano haya.
Gradel alifunga kutoka umbali wa yadi 20, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa Tembo hao. Wengine watakaovuka kwenye kundi hili wataamuliwa kwa kura, baada ya Mali na Guinea kufungana kwa kila namna.
Nchi mbili hizo zinapinga mfumo wa kutumia kura kupata anayefuzu, zikitaka mshindi apatikane uwanjani kwa kurudiana, ikishindikana wapigiane mikwaju ya penati. Mali walikwenda sare ya 1-1.
Edgar Salli wa Cameroon atakuwa mwenye uchungu zaidi, kwa sababu alikosa anfasi mboili nzuri za kusawazisha akiwa ndani ya eneo la penati. Ivory Coast walionekana kuwa wazuri, ambapo bekiSerge Aurier alimtilia majalo Wilfried Bony lakini kipa Fabrice Ondoa akaokoa hatari.
Kuvuka kwa Ivory Coast kumepokewa kwa masikitiko na mabingwa watetezi wa England, Manchester City ambao walikuwa wameshajiandaa kukodi ndege kuwasafirisha Yaya Toure na Bony kurudi England kwa ajili ya mechi ngumu dhidi ya Chelsea wikiendi hii.
City walifungwa na Arsenal kwenye mechi iliyopita, hivyo wapo katika wakati mgumu wa kutetea taji, wakiwa na upungufu wa pointi tano nyuma ya Chelsea. Hata hivyo, Chelsea nao wapo hatarini kumkosa Diego Costa aliyeshitakiwa kwa kumrukia na kumkanyaga mchezai wa timu pinzani. Cesc Fabregas naye ana matatizo ya utimamu wa mwili.