Jose Mourinho baada ya msimu jana kuisha alitabainisha kuwa katika
dirisha hili la usajili atasaini wachezaji wanne tu.
Ila kwa taarifa zilizotoka jana zilionesha kuwa atasaini wachezaji
watatu tu kutokana na hali ya bei za wachezaji kwenye soko la usajili.
Mpaka sasa hivi ameshasajili wachezaji wawili ambao ni Lukaku pamoja
na Victor lindelof, hivo kwa mujibu wake atakuwa amebakiza mchezaji
mmoja tu.
Swali kubwa ni nani ambaye anastahili kuwa kama mchezaji wa mwisho
kusajili katika kipindi hiki cha usajili kwa Manchester United?
Kabla ya kuanisha mchezaji ambaye anastahili kuwa mchezaji wa mwisho
kama mchezaji wa mwisho kusajili, tunatakiwa kujiuliza ni eneo lipi
ambalo lilikuwa lina matatizo msimu jana kwa Manchester United?
Msimu jana, Manchester United ilikuwa imara sana kuanzia eneo la
nyuma mpaka eneo la kiungo ambalo lilihusika sana kutengeneza nafasi
nyingi za kufunga magoli lakini tatizo kubwa lilikuwa kwenye eneo la
ushambuliaji.
Pamoja na kwamba Zlatan alihusika kwenye magoli mengi msimu jana
lakini pia alipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Hivo tatizo kubwa la Manchester United lilikuwa eneo la ushambuliaji,
na Jose Mourinho ameliona hilo ndiyo maana akamleta Lukaku ambaye
msimu uliopita alifunga magoli 25+ kwenye klabu ya Everton.
Kumleta mfungaji pekee haitoshi, anatakiwa mtu ambaye anauwezo wa
kutengeneza nafasi nyingi za magoli pamoja na kufunga goli nyingi
Msimu uliopita alifunga goli 11 na kutoa msaada wa magoli 8, hii
inaonesha kumleta Ivan Perisic unakuwa unaleta magoli kuanzia kumi na
pasi za msaada wa magoli 8 kitu ambacho ukijumlisha na goli za lukaku
unakuwa na uhakika wa magoli 35+ na pasi za msaada za magoli 20+ kwa
wachezaji wawili pekee.
Pia Ivan Perisic anauwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa
pembeni,kushoto na kulia.
Sehemu ambazo mtu kama Ashley Young alikuwa akizitumikia vzuri.
Pia hii inaweza ikawapa nafasi Martial na Ivan Perisic kucheza kwa
pamoja kwa sababu mmoja anaweza kucheza kulia na mwingine kushoto na
wakawa wanabadilishana.
Pia Ivan Perisic ana uwezo wa kucheza kama namba kumi .Hivo anauwezo
wa kucheza nafasi tatu kwa ufasaha kitu ambacho kitakuwa na msaada
mkubwa kwenye timu