Menu
in

IHEFU IKIFIKA MBALI BASI SOKA LETU LITAKUWA

IHEFU FC

IHEFU FC

Klabu ya Ihefu ni mojawapo ya klabu changa sana nchini ila yenye mafanikio. Klabu hii imepanda daraja katika msimu huu wa ligi kuu bara Tanzania. Klabu hii ina maskani yake katika ardhi ya walima mchele maeneo ya Mbaralli mjini Mbeya . timu hii ni mojawapo ya vilabu ambavyo vimethubutu kujenga kiwanja chake chenyewe licha ya kwamba kiwanja hicho kilionekana kama hakina kiwango kikubwa sana

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mtandaoni klabu hii ilianza ujenzi wake wa kiwanja mnamo juni 2020 na yasemekana uwanja wao una uwezo wa kuingiza watu 5000 mpaka 6000 ndani ya wakati mmoja. Uwanja wao wa nyumbani unajulikana kama highland estates stadium  ambao upo Mbarali. Kauli mbiu yao ni maneno kidogo kazi zaidi. 

Kwa mujibu wa vyanzo vya mtandaoni vinaonyesha kilabu hichi ni mali ya kampuni tanzu ya Highland estates ambayo ni mjumuiko wa makampuni kadhaa ambayo yanafaya biashara kadhaa ikiwemo ujenzi na upangishwaji wa majumba, ulimaji wa mazao ya chakula,usafirishaji, uuzaji wa mashine, kiwanda cha maji, 

Kilabu hichi kilipoingia ligi kuu kilianza kwa hali mbaya kwani matokeo yao uwanajani hayakuwa mazuri na hili lilipelekea kuamua kuachana na kocha wao na hatimaye kuamua kumchukua aliyekuwa kocha wa timu ya Mtibwa Sugar Zuberi Katwila kuwa kocha wa timu yao. Timu hiyo ikafanikiwa kupata mafanikio kiasi cha kuifanya klabu hiyo ionekane kuwa inaweza ikasalia kwenye ligi kuu.

Kwa muono wangu klabu hii msimu huu haiwezi kuwa na maajabu sana kwani kasi(momentum) iliyoanza nayo ni ndogo sana kwa hiyo imepelekea kilabu hicho kuwa na wakati mgumu kwa kutumia mda mwingi kuanza kutafuta matokeo ambayo yataifanya klabu hiyo kuweza kubaki katika ligi kuu badala ya kuwa na matokeo yatayoweza kuivusha klabu hiyo na kuifanya kubeba ligi na kuwa ni mojawapo ya vilabu vyenye kugombania ubingwa na hatimaye kupambania kushiriki kwenye mashindano makubwa barani afrika.

Kilabu hichi kwa sasa kinatakiwa kijipanue katika idara ya masoko ili kiweze kijitengenezee wigo wa mashabiki(fan base) ili kiweze kutengeneza wigo wa mapato.

Kilabu hichi kinaweza kutumia modeli/mfumo ambao walitumia kilabu cha uingereza cha Leicester city katika msimu wa mwaka 2015/2016 ambapo walimchukua kocha mwenye uzoefu katika ligi kuu za ulaya yaani namzungumzia Claudio Ranieri. Ranieri hakupewa bajeti kubwa ya usajili ila alipewa wachezaji wenye ari ya kutaka kufanya makubwa. Naona Ihefu wao wameamua kumchukua Katwila ambaye ana uzoefu wa miaka kadhaa wa ligi ya Tanzania kwa ajili ya kukinoa kikosi chao. Wanachotakiwa kukifanya ni kujaribu kumpatia mda Katwila akimoe kikosi chao na kama akiweza kukifanya kikabaki katika ligi kuu basi apewe nafasi katika msimu ujao.

Binafsi naona kama Ihefu itafanikiwa kufika mbali itaweza kuleta mageuzi katika soka la Tanzania najua wengi watashangaa kwa nini sioni mafanikio ya uwekezaji wa Mohammed Dewji katika Simba mpaka niangalie uwekezaji wa Ihefu jijini Mbeya. Kwanza Dewji ameichukua Simba tayari ikiwa imeshakuwa nembo kubwa barani afrika kwani ameikuta klabu ikiwa inakadiriwa ina mashabiki zaidi ya milioni 10. Hao wawekezaji wa Ihefu wameanza na klabu ikiwa katika hali ndogo sana na wamepambana mpaka klabu imefika katika hatua ya kuingia katika ligi kuu bara. Mo alijaribu kusimamia kilabu kidogo cha African Lyon na kujaribu kuifanya klabu kubwa na alishindwa na si hilo tu aliwahi kujaribu kusimamia kilabu cha Singida United na alishindwa.

Mafanikio ya Ihefu yatafanya wawekezaji wengine wasiogope kuwekeza kwenye mpira na hususani kuwekeza kwenye timu ndogo. Wataona mafanikio hayo kama ni chachu ya wao kuweza kuingia kwenye ulingo wa kusimamia vilabu hivyo. Wamiliki wa Ihefu wameamua kufanya maamuzi magumu kama aliyoyafanya mmiliki wa Leicester au walivyofanya wamiliki wa kilabu cha Manchester City pindi walipoamua kuchukua hatamu za uongozi wa kilabu hicho. Natamani niione siku moja klabu ya Ihefu ikishiriki mashindano makubwa barani afrika ikiwemo klabu bingwa barani afrika.

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

Leave a Reply

Exit mobile version