Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amewataka viongozi wa klabu za Tanzania kuiga mfano wa Ulaya katika kufanya usajili wa wachezaji wao.
Tenga aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ukocha yalioandaliwa na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambapo wachezaji wengi wa zamani walijitokeza katika mafunzo hayo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shadrack Nsajigwa, Edibily Lunyamila, , Ally Yusuph ‘Tigana’, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Seleman Matola na wengineo.
Kauli hiyo ya Tenga imekuja wakati timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zipo katika kipindi cha usajili wa wachezaji wao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi hiyo inayotarajia kuanza Agosti 24.
Tenga alisema kuwa hana huakika kama kweli viongozi wanawapima wachezaji wao afya kabla ya kuwasajili ila katika kanuni za usajili kanuni hiyo hiyo.
Pia Tenga alisema kanuni hiyo itaanza kufanya kazi msimu ujao ambapo itaambatana na kanuni ya kusajili wachezaji watatu tu wa kigeni ilikuweza kuwapa nafasi wachezaji wa ndani ambao ndio wanatengeneza timu ya Taifa.
Alisema kanuni hiyo imekuwa haifuatwi na wahusika hivyo wanataka kuiongezea msisitizo na makali iliiheshimiwe na kila klabu kuakikisha hawasaili wachezaji wagonjwa ambao hawawezi kuwasaidia katika timu zao.
Aliongeza kuwa,utamaduni sasa wa viongozi na wanachama kufanya kazi ya usajili ndiyo unapelekea klabu kutofikia malengo yake kutokana na kuwa wachezaji wasiokuwa na uwezo.
Hata hivyo Tenga alisisitiza umuhimu wa klabu kuwatumia wachezaji vijana akisema ndiyo njia sahihi ya kupata mafanikio.
Hata hivyo kwa upande wa klabu zenyewe zilisema kuwa wao wamekuwa wakitekeleza kanuni hiyo kwa asilimia miamoja.
Kwa upande wa kocha wa Simba Abdallah ‘King’ Kibadeni alisema kuwa yeye kwa upande wake achukui mchezaji bila kupimwa na daktari wao na kujirizisha kuwa ni mzima atamfaa.
Alisema tayari amefanya hivyo kwa wachezaji wake mbali mbali akiwemo beki raia wa Uganda Samweli Senkoomi ambaye amesajiliwa hivi karibuni na amajiridhisha kuwa yupo fiti na kuanza naye mazoezi.
Kwa Upande wa Yanga Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Bin Kleb alisema kuwa anaona kama Tenga amechelewa kutoa tamko hilo kwani wao walikwisha anza siku nyingi na ndio maana mpaka sasa wamekuwa na kikosi imara ambacho hakina majeruhi wa kudumu.
Azam kupitia kwa Meneja wa timu yao Patrick Kahemale alisema wao wamekuwa wakifanya kwa wachezaji wa kigeni kabla ya kujiunga katika timu yao.
Pamoja na viongozi hao kudai kuwa wanawafanyia vipimo wachezaji wao lakini bado kumekuwa na tatizo kubwa la kuwa na wachezaji majeruhi wa kudumu katika klabu hizo.
Hata hivyo Tenga amewataka makocha wa klabu za soka nchi wawe mstari wa mbele katika kupinga vitengo vya upangaji matokeo katika mechi.
Alisema,endapo vitendo vya udanganyifu havitapigwa vita na kila mdau wa soka itakuwa viguu nchi kupiga hatua ya kimaendeleo.
“Udanyanyifu ni jambo baya sana katika mchezo wao soka,nawaombeni huko mnakoenda kufundisha muwe mstari wa mbele kupiga vita tabia hii mbaya,”.alisema Tenga na kuongeza: