Miaka mingi imepita, mechi nyingi zimechezwa na wamekutana katika
viwanja mbalimbali lakini mwisho wa siku Arsene Wenger alikuwa mnyonge
mbele ya Jose Mourinho.
Jana ilikuwa siku nzuri kwa Arsenal, siku ambayo timu ilicheza vizuri
sana na kuwezesha Arsene Wenger avunje mwiko wa kutomfunga Jose
Mourinho.
Kuna kitu kimeanza kuonekana kwenye mfumo huu wa 3-4-2-1 ambao Arsene
Wenger ameanza kuutumia hivi karibuni.
Ingawa mechi ya jana haikuwa kipimo sahihi kwa eneo la kujilinda la
Arsenal kwa sababu ya aina ya timu ambayo walikuwa wanacheza nayo
ambayo ilikuwa imekosa mshambuliaji wa kariba ya juu lakini ukweli ni
kwamba kuna mabadiliko makubwa kwenye eneo hili.
Holding pamoja na umri wake kuwa mdogo lakini ni mchezaji ambaye
amekomaa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal kwa sababu ni
mtulivu sana anapozuia mashambulizi pia ana uwezo mzuri wa kuanzisha
mashambulizi.
Gibbs anaonekana na faida kubwa kwenye eneo la ulinzi zaidi kuliko
eneo la kushambulia. Anajilinda vizuri sana na ule upande wa kushoto
ambao wanacheza na Nacho Monreal wametengeneza ulinzi dhabiti lakini
tatizo moja ni kwamba Gibbs hana krosi nzuri zenye madhara kwa
mpinzani.
Oxlaide Chamberlain ni mzuri sana kwa upande wa kulia hasa hasa
anaposhambulia, ana krosi zenye madhara makubwa sana kwa mpinzani na
anakasi nzuri, lakini tatizo lake ni moja tu ana uwezo hafifu wa
kurudi nyuma kusaidia kukaba, kama Manchester United wangekuwa na
Winger mwenye kasi jana ule upande wa kulia mwa Arsenal ndiko kulikuwa
na nafasi kubwa ya kuwaulia Arsenal.
Inawezekana kabisaa Pogba jana alikosekana na umuhimu wake ulionekana.
Mata hakuweza kuunganisha vizuri eneo la kiungo na eneo la
ushambuliaji.
Viungo wa Arsenal jana walikuwa na mchezo mzuri sana hivo alitakiwa
mtu ambaye anauwezo wa kuchukua mpira na kukimbia nao au kupiga pasi
kuelekea kwenye lango la Arsenal .
Xhaka na Ramsey walicheza vizuri sana, Xhaka alikaba vizuri na Ramsey
alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukimbia kutoka eneo la Arsenal mpaka
eneo la Manchester United.
Na ubora wa kiungo cha Arsenal ulichagizwa na Ozil pia kucheza katika
eneo huru ambalo lilimfanya awe na uwezo wa kuchezesha timu kwa kupiga
pasi hivo kuifanya timu iwe na mpira muda mwingi.
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa Sanchez kupunguza magoli kupitia mfumo
huu wa 3-4-2-1 kwa sababu anacheza katika eneo huru eneo ambalo
ƙlinamfanya awe sehemu nyingi mwa uwanja na kuwa mbali na eneo la kumi
na nane la timu pinzani hivo .
Na hii taratibu inaonesha ni jinsi gani mfumo huu unatua mzigo
aliokuwa ameubeba Sanchez kwa muda mrefu kwa kuibeba Arsenal.
Muda huu timu inaundwa kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake
ipasavyo na haimzunguki mtu kwa asilimia kubwa.
Kasi ya Welbeck ilikuwa inawafanya mabeki wa Manchester United
wakimbie kurudi nyuma na siyo kwenda mbele kitu ambacho kilisababisha
wao kushindwa kupandisha timu .
Muda mwingi Manchester United walikuwa nyuma ya mpira na walijizuia
vizuri hata aina ya magoli waliyofungwa ni magoli ambayo hayakutokana
na makosa binafsi ya mabeki au wachezaji wa timu ya Manchester United
ila walifungwa magoli ambayo timu nyingi zenye ukuta mgumu hufungwa.
Tuanzabe ni moja ya mabeki wazuri wa kati wanaokuja