KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Marcio Maximo amesema Watanzania ndio watakaoamua hatma yake kuendelea na kibarua ama la.
Akizungumza na Mwananchi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana baada ya kuwasili kutoka Ivory Coast ilikokuwa ikishiriki fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani, CHAN, Maximo alisema anaipenda Tanzania na anapenda kuona jinsi inavyobadilika kisoka.
Katika siku za karibuni kumekuwepo na mijadala mbalimbali kuhusu kuendelea ama kusitishwa kwa mkataba wa Maximo wa kuinoa Stars. Mkataba wa kocha huyo unamalizika baadaye Julai.
Kipaumbele changu cha kwanza ni maendeleo ya soka katikaTanzania. Napenda jinsi watu wanavyoipokea timu yao, hata wachezaji wanabadilika, nidhamu iko juu sasa watakaoamua mimi niwepo ni Watanzaniaî.
‘Nina mipango mingi ya maendeleo, nina programu mbalimbali, nataka kutengeneza soka ya kisasa na wachezaji wajitambue kuwa soka kwa sasa ni ya kulipwa na watambue kuwa kuna soka ya kulipwa ambayo inaweza kuwafaa katika maisha yao,’ alisema.
Maximo alisema walikwenda Ivory Coast kushindana na si kushiriki kwani walijitahidi kwa kila hali, lakini baadaye bahatÌ haikuwa yao.
Alisema soka Afrika inachezwa na kwamba si Afrika Magharibi pekee, kanda zote za Afrika ziko juu.
Akiwazungumzia wachezaji wake, Haruna Moshi ëBoban na Athumani Idd ëChujií ambao imeelezwa kuwa na misigano nao, Maximo alisema kuwa wachezaji hao hawana nidhamu na wameshindwa kufuata masharti na taratibu za timu.
‘Mimi siangalii jina wala uwezo wa mchezaji, kama mtu hana nidhamu ndani na nje ya uwanja lazima ataondoka kwenye timu yangu.’
Mwananchi ilipomuuliza kama huo ndio mwisho wao Stars, Maximo alijibu: ‘Tutaangalia mbele ya safari, acha kwanza Ijumaa (kesho) nitatangaza timu ya kucheza na Vancouver Whitecaps ya Canada, nitataja sura mpya nyingi.’
Stars iliwasili jana na kulakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera ambaye aliwapongeza na kuwakaribisha nyumbani wachezaji.
Kazi yenu tumeiona, mmecheza kwa nguvu lakini tukubali matokeo kwamba katika soka kuna kushinda, kufungwa na sare na ndiyo matokeo mliyokuja nayo ukweli tumeshangilia dakika mbili lakini tukahuzunika dakika mbili baadaye, alisema.
Awali, mkuu wa msafara, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Muhammed Seif Khatib alisema: Nia ilikuwa kufika mbali na kutwaa kombe lakini vijana wamepigana kadiri ya uwezo wao na bahati haikuwa yao.’
Nahodha wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa akitoa neno lake, alisema mashindano yalikuwa magumu na mechi mfululizo zimewapa somo.
‘Naamini programu zikiendelea, huko mbele tutafanya vizuri zaidi nawapongeza wote waliotuwezesha hata kufikia hapa,’ alisema.