Menu
in , , ,

Harry Redknapp aachia ngazi QPR

Kocha wa Queen Park Rangers (QPR), Harry Redknapp ameachia ngazi klabuni hapo, siku moja tu baada ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili nchini England.

Taarifa zinasema kwamba uamuzi wake wa kuachia ngazi umekubaliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya QPR, ambayo timu yao ipo katika hali mbaya Ligi Kuu ya England (EPL), wakipigana kuepuka kushuka daraja.

Licha ya kusajili wachezaji wazuri, wakiwamo ambeki Rio Ferdinand na Steven Caulker, mambo yameenda kombo kwa klabu hiyo ya London.

Redknapp ni bosi wa zamani wa Tottenham Hotsopur ambako alifukuzwa kazi baada ya uongozi kudai alishindwa kuwapatia nafasi kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), huku wakisema walitaka kocha mwenye mvuto zaidi, ndipo wakampata Andre Villas-Boas ambaye hakufanya vizuri wala.

Amepata pia kuwafundisha West Ham. Amekuwa QPR tangu 2012, ambapo alipewa kazi ya kuzuia kushuka daraja, akashindwa hivyo akashuka nao na kuwapandisha msimu uliopita. Kati ya watu watakaokumbukwa kusajiliwa hapo na Redknapp, ni beki Christopher Samba, ambaye alikuwa ghali na aliboronga, akichangia kuanguka kwa timu hiyo.

Kocha huyu jina lake kamili ni Henry James ‘Harry’ Redknapp aliyezaliwa Machi 2, 1947 na alipochukua kazi yake aliyoacha, wengi walichukulia kwamba angekuwa na mafanikio, na huenda ingekuwa ya mwisho katika soka ya ushindaji ya daraja la juu.

Amefundisha kwa muda mrefu soka, ikiwa ni tangu 1983 alipokuwa na Bournemouth na ndiye kocha mwenye umri mkubwa zaidi katika medani ya soka ya kulipwa nchini England.

Timu nyingine alizofundisha ni Portsmouth (nyakati mbili tofauti), na Southampton. Katika msimu wake wa 2009/10, Redknapp, raia wa Uingereza aliwapeleka Spurs kwenye michuano ya UCL kwa mara ya kwanza kwa timu hiyo kwenye historia.

Mwanawe, Jamie Redknapp, alicheza Bournemouth na Southampton huku baba yake akiwa bosi hapo. Redknapp pia ni mjomba wa kiungo wa zamani wa Chelsea na sasa Manchester City, Frank Lampard, aliyecheza chini yake pia enzi za West Ham.

Mmiliki wa QPR, Tony Fernandes amekuwa wakati wote akieleza kuwa na imani na Redknapp na kwamba hapakuwapo mpango wowote wa kumfuta kazi. Anaondoka akiwaacha QPR wakiwa katika nafasi ya 19, moja toka mkiani, wakiwa na pointi 17 kutokana na mechi 23.

QPR wana mizania ya mabao -18, mbaya kuliko wa klabu nyingine yoyote ya EPL. Wanaoshika mkia ni Leicester wenye pointi 17 na mizania ya mabao -16. Wakati yakiwa hivyo huko mkiani, Chelsea wanaongoza ligi wakiwa na pointi 53 kutokana na idadi hiyo hiyo ya mechi 23 na mizania nene ya mabao 32.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version