Mancahester United haihitaji mabadiliko sana endapo wakimbakisha nyota wao Paul Pogba kikosini.
Hapo nyuma kulizuka tetesi kuwa kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na Manchester United Paul Pogba huenda akatimkia Real Madrid mwishoni mwa msimu.
Hii ilitokana na kutoelewana na viongozi pamoja na benchi la ufundi nyota huyo iliaminika hakuwa na furaha ndani ya kikosi huko.
Hizi ni tetesi tu hazina uhakika kamili, ila juu ya hizo tetesi bado shabiki wa Manchester United hawakuwa wanampenda nyota huyo kwa uvumi wa habari hizo wakitaka aondoke ili wapewe nafasi wachezaji wenginie, hapa hawajajali kiwango cha nyota huyo.
Huenda hawajui kuwa umuhimu wa Pogba anayeujua shabiki wa timu nyingine kabisa lakini pia hawaangalii wakati uliopo sasa kuna nani pale mbele.
Tuanzie hapa sasa, kocha mkuu wa timu huyo Solskajaer hakupewa fedha nyingine za usajili, timu ilikuwa inacheza vibaya kwakuwa hakukuwa na watu watakaoweka chachandu pale mbele.
Solskajaer alihitaji huduma ya Bruno Fernandez kitambo sana ila hakuipata, hatimaye baadae viongozi wakaamua kumnunua na kumpa kandarasi la kuitumikia timu hiyo kwa matakwa ya kocha.
Bahati nzuri Bruno Fernandez ameingia moja kwa moja kikosi cha kwanza na kuonesha kiwango cha hali ya juu.
Endapo Pogba wakimbakisha basi timu hiyo itakuwa kiboko kwani nachelea kusema hivyo bila ya uwoga kwa kuangalia muunganiko wa Pogba na Fernandez.
Viungo hawa wote wawili mafundi sana kila mmoja anafaida yake wakati timu inapokuwa na mpira na isipokuwa na mpira.
Pogba yeye amekamilika kama mpira anao adui utaona kazi atakayofanya wakati huo mpira wakimiliki wao utaona atakavyobadilika kama kinyonga na kushambulia kwa nguvu sana.
Kwa upande wa Bruno timu inapokuwa na mpira anafanya kazi yake kwa asilimia mia moja na madhara yake makubwa hasa kupiga mashuti ya mbali.
Hawa wote wanauwezo wakucheza shimoni kwa maana namba 10 lakini pia unayo sababu ya kufurahi kwani unaweza kumtumia Pogba kama namba nane na akakupa kile unacho kihitaji.
Uwezo wa nyota hao umedhihirika pale alipoingia Pogba na kucheza kwa dakika 33 akionesha kiwango cha hali ya juu akisababisha penati ambayo Bruno amefunga.
Lakini zile ‘penetration pass’ za nyota huyo kutoka taifa la Ufaransa bado zipo na zina madhara makubwa kwa timu pinzani.
Labda kwa shabiki wa Manchester Unites ambaye hajui thamani ya Pogba na akiomba aondoke kutokana na malingo yake basi asiombe dua hiyo kwani yajayo yanafurahisha kwa watu hao wawili.
Hivi unaonaje siku Solskajaer akipanga hivi kikosi chake, De Gea, Wan Bisaka, Shaw, Eric Baily, Maguire, Fredy, James, Pogba, Rashford, Bruno na Martial unadhani balaa lake litakuwaje hapa.
Kikosi cha akiba utakipanga wewe mwenyewe ukianzia na Ighalo, Greenwood, Matic, Mac Tominay na Dalot.
Marekebisho ambayo nayaona ndani ya timu hiyo ni sehemu ya ulinzi apatikane beki mmoja aliye na uwezo kama wa Maguire au Baily, tatizo la mchezaji huyo wa Ivory Coast majeruhi hivyo kama akipatikana mtu anayeweza kukaa kwa mechi nyingi bila maumivu ingependeza zaidi.
Pia aongeze kiungo mwingine damu mbichi maana Matic jua linaelekea kuzama hivyo wapate kiungo mkabaji asaidiane na Fredy pamoja na Scott Mac Tominay
Beki wa kushoto aliye mzima acheze na Luke Show hapa nako kuna tatizo japo si sana.
Na winga mmoja ili akimbie sana upande huo mana kuna baadhi ya nyota wa timu hiyo hawana mtiririko mzuri siku wanafika malengo siku nyingine wanaboronga.
Mwisho kabisa aongezee nguvu katika safu ya ushambuliaji ili sasa ikija ile mipira ya Pogba afunge.
Waliopo kwangu mimi hawajafikia malengo, si muingizi Ighalo kwakuwa mkopo wake umeongezwa hadi mwezi Januari mwakani ila bonge la mshambuliaji.
Kama ningekuwa kocha wa Manchester United basi ningejaribu kuchukua wachezaji watano kuunganisha na wale wa zamani mabadiliko yangeonekana kiutendaji ndani ya uwanja.
Ila katika hao watano dirisha kubwa angeanza na wachezaji 3 waliobaki watamaliziwa dirisha dogo.
Hiyo ingewapa jeuri wapenzi na mashabiki wa Manchester United.
Nakuhakikishia kuwa baada ya kumaliza kwa mechi zilizobaki utakuja kuhadithia umuhimu wa Pogba na Bruno.