Michezo imekuwa sehemu kubwa ya ulimwengu inayotazamwa na kama ikihitaji kufanya ‘Promotion’ ya jambo lolote linapata watazamaji wengi sana.
Michezo ni furaha, amani, kinga pamoja na dawa kwa vitendo viovu kama vya ubaguzi wa rangi na kuuliwa kwa watu weusi pasipo na hatia.
Kinachoendelea duniani kwa sasa kifo cha Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd aliyeuawa na jeshi la polisi kwa kukandamizwa shingo na kukosa punzi.
Nyota wa zamani wa Arsenal na sasa anachezea Chelsea raia wa Ufaransa emeonekana kupinga ubaguzi wa wowote unaoendelea duniani na vitendo vya kuuliwa kwa watu weusi.
Giroud ameonesha kusikitishwa na vitendo vyote vya ubaguzi ikiwemo ule wa rangi na tukio linaendelea Floyd.
Yeye baada ya kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Aston Villa ametoa heshima hiyo kwa kupiga magoti na kuonesha mikono yake juu akiashiria kuomba kwa Mungu matukio kama hayo yasitokee tena.
Alipoulizwa na vyombo anuwai vya habari nchini England alisema kuwa ilikuwa anatoa heshima kwa Floyd na ile kampeni ya ‘Black Lives Matter’