Menu
in , , ,

Ghana waangukia pua

*Nigeria, Iran sare ya kwanza

Ghana wameshindwa kuendeleza rekodi ya kuwatoa Marekani kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Ghana wamekubali kichapo cha mabao 2-1, wakiwa kwenye kundi gumu lenye timu za Ujerumani na Ureno. Waliruhusu bao la kwanza sekunde ya 29 tu kupitia kwa Clint Dempsey.

Mchezo ulikuwa mkali na nusura timu zitoke sare kama si John Brooks kufanikiwa kutumbukiza kwa kichwa mpira katika dakika za mwisho mwisho.

Dempsey alitumia akili ya haraka mpira ulipoanza ambapo alimtoka John Boye kabla ya kutikisa nyavu.

Ghana walimudu kuhimili kasi ya Marekani wanaofundishwa na mpachika mabao wa zamani wa Ujerumani, Jurgen Klinsman kwa kusawazisha kupitia kwa Andre Ayew aliyedokolewa mpira kwa kisigino na Asamoah Gyan.

Dakika za mwisho Marekani walionekana kuchoka, lakini Brooks (21) mzaliwa wa Ujerumani anayecheza beki ya kati, alisogea mbele baada ya Ghana kutoa mpira wa kona kizembe, akapachika bao yadi tatu kutoka golini.

Ghana ndio waliwatoa Marekani mara mbili kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006 na 2010.

HISTORIA MPYA YA SARE 2014

Wawakilishi wengine wa Afrika, Nigeria, waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele hawakuanza vyema.

Nigeria wametoka suluhu na Iran, ambayo ni ya kwanza katika fainali za mwaka huu. Iran walifurahia matokeo hayo.

Nigeria walitawala mchezo kwa karibu asilimia 70 lakini hawakuweza kuipenya ngome ya Iran ambao hawakuwa wakipewa nafasi ya kufanya vyema.

Katika mechi ya kwanza ya kundi hili, Argentina waliwafunga kwa tabu Bosnia-Hercegovina 2-1.
Mabingwa hao wa Afrika walipata nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza lakini Ogenyi Onazi alipiga yadi moja nje ya goli.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version