Feisal Salum ama Fei Toto kwa sasa ndio mchezaji ambaye amekuwa kila analolifanya lazima lijadiliwe katika soka la tanzania bara miongoni mwa wachezaji wa ndani. Mchezaji huyu amekuwa anashika vichwa vya habari vya nchini tanzania kuanzia kwenye magazeti mpaka kwenye mitandao ya kijamii kwa mda kidogo. mchezaji huyo aliyekulia visiwani Zazibar kwa sasa anachezea matajiri wa kitongoji cha Mbagala Chamanzi klabu ya Azam football club.
Fei Toto alisajiliwa mnamo Januari 11 mwaka 1998 na kwa sasa ana umri wa miaka 26. mchezaji huyu soka lake la kulipwa alilianza katika klabu ya JKU ya zanzibar ambapo alicheza kutoka mwaka 2016 mpaka mwaka 2018. alicheza hapo kwa mafanikio na alionekana sana kwenye mashindano ya Mapinduzi ambapo aling’ara kwenye mashindano hayo na hivyo kupelekea vilabu mbalimbali vikubwa kumuona na hapo ndipo kinyang’anyiro cha kuisaka saini yake kilipoanza. baada ya hali ya kuvutiwa na kipaji chake ndipo Yanga waliweza kuidaka saini yake baada ya kusajiliwa na klabu ya Singida United ambayo nayo ilimpeleka Yanga.
Mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi za kimataifa 36 na amefunga magoli 2mafanikio yake yalipatikana zaidi katika klabu ya Yanga ambapo alisaidia klabu hiyo kubeba mataji ya ligi kuu tanzania bara na kombe la FA. mechi yake ya kwanza ya kimataifa ilikuwa mechi ya hatua ya kufuzu mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika (AFCON) ambayo ilichezwa mnamo oktoba 16 dhidi ya Cape Verde. kucheza kwake vizuri kulimsaidia kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ambacho kilishiriki mashindano ya AFCON ya mwaka 2019.
Kocha Emannuel Amunike ambaye aliyekuwa kocha wa timu ya taifa wa wakati huo alishangaa ni kwa nini Fei Toto hachezi klabu ya Barcelona ya uhispani na kauli hiyo alitoa hadharani na iliwashitua watu wengi sana kwani wengi walimuona kama hana kiwango hicho. Watu walimshutumu Amunike kwamba amekosea kutoa kauli hiyo na wala Amunike hakuwahi kuomba radhi kwa kauli yake hiyo. Msimu ulifouata katika klabu ya Yanga alikuja kocha Nasreddine Nabi kwa ajili ya kuifundisha klabu hiyo na katika nyakati za kocha Nabi ndipo Fei Toto alizidi Kung’ara na kuwa ni mchezaji ambaye alikuwa anapata nafasi Zaidi katika nafasi ya kiungo mshambuliaji. Fei alisumbua timu pinzani kwa magoli hususani magoli ya mashuti makali nje ya 18 na pia alisaidia sana kutoa assisti ambazo zilizaa magoli muhimu.
Msimu uliopita ulianza vizuri kwa Fei Toto na ilipomalizika mzunguko wa kwanza wa ligi zilianza tetesi kwamba alikuwa ameshamalizana na klabu ya Azam na hivyo akawa haendei tena mazoezini kwenye klabu ya Yanga na alikuwa hata kambini hatokei. Hazikupita siku nyingi wadau wa soka wakasikia taarifa kwamba alikuwa ameingiza kwenye akaunti ya klabu ya Yanga kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake ili awe mchezaji huru ili asaini kuwatumikia wababe hao wa Chamanzi. Tukio hilo lilizua mvutano baina ya Uongozi wa Yanga nay eye kwani uongozi haukubariki kitendo hicho na ulikuwa unadai kwamba bado yeye ni mchezaji halali wa Yanga na uliendelea kuingiza hela katika akaunti yake kwa kuashiria kwamba bado ni mchezaji wao. Mvutano huo ulimfanya aende kushitaki TFF ili iingilie kati na kuvunja mkataba wake huo.
Suala hili lilisisimua sana wadau wa michezo na likawa ni mjadala mkubwa sana kwani watu wengi walitamanai kuona hatima ya mzozo huo. Mzozo huo uliwahi pia kumuibua mama yake mzazi Fei Toto ambaye alitoa madai yake hadharani kwamba mchezaji wake alikuwa anadhalilika katika klabu hiyo na kwamba ilifikia hatua mpaka alikuwa anapewa chakula cha ugali bila ya mboga na wakati mwingine alikuwa anapewa ugali na sukari.Mzozo ulichukua miezi kadhaa na hatimaye mwishoni klabu ya Yanga ilikubali kumwachia kwa pesa ya usajili ambayo hawakuiweka wazi na Fei toto akawa huru kuitumikia Azam katika msimu huu ambao ndio kwanza umeisha.
Msimu ulipoanza alitambulishwa kama mchezaji wa Azam na akaanza kuitumikia klabu hiyo na katika mechi yake ya kwanza ambayo walicheza dhidi ya Tabora United ambapo walikuwa uwanja wa nyumbani pale Azam Complex alifunga magoli kadhaa na akajikuta ameanza msimu vizuri kwa kuanza kwa mfungaji anayeongoza kwa mabao mengi. Alidumu kama mfungaji bora kwa miezi kadhaa mpaka pale kiungo mshambuliaji wa Yanga na taifa la Burkina Faso bwana Aziz ki alipoanza naye kufunga magoli kwa kasi na hatimaye ukazaliwa ushindani baina yake na Aziz Ki ambao ulienda hadi mechi ya mwisho ya msimu ambapo Aziz Ki alifunga mabao mawili na hivyo kufanya kumzidi Fei toto na hivyo kufanikiwa kuwa ndio mfungaji bora wa msimu.
Alisaidia klabu yake ya Azam kuwa mshindi wa pili wa ligi na kuingia pia fainali ya kombe la CRDB CONFEDERATION CUP ambapo katika mechi hiyo walifungwa kwa penati na klabu ya Yanga ambapo picha ya Fei toto ilitawala kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kwa mashabiki wengi wakimjadili yeye na kiwango alichokionyesha. Mpende ama mchukie Fei Toto lakini ndio mchezaji mzawa ambaye anajadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii na katika vijiwe vya soka kwa sasa.