kushuka na kupanda kwa England
Tangu Juni 2020, wachezaji wengi wamekuwa na mtindo wa kupiga goti moja kama njia ya kuunga mkono usawa wa rangi na kupiga vita ubaguzi wa rangi, vitendo ambavyo vilitawala kwenye soka.
Hivi sasa tunashuhudia kwamba ni asilimia nne tu ya makocha katika Ligi Kuu ya England ni weusi na baada ya England kupoteza kwenye michuano ya Euro mwaka jana, wachezaji watatu weusi waliopiga penati walibaguliwa mtandaoni kutokana na rangi yao nyeusi.
Mwaka 1990, wachezaji weusi walicheza huku wakibaguliwa, Paul Parker anasema.
“Kuna watu wachache ambao hawakupenda hili, lakini walikuwa wachache kuliko wa leo hii.”
Je, uliungwa mkono na wachezaji weupe? “Hapana. Wala hatungalitarajia hilo. Tulishughulika nalo wenyewe kwa kuwa imara kiakili na kujiamini na pia kuwapuuza. Je, kulikuwapo ubaguzi wowote ndani ya kikosi cha England? “Hapana, si kwa hata miaka milioni.”
Kama ilivyo kwa wachezaji weusi wengine wachache wa kizazi hicho waliosonga mbele na kuwa makocha, Parker naye alifanya hivyo katika ngazi za chini, akiwa na Chelmsford City na Welling United.
“Lakini haikuwa yangu. Sikufurahia kufanya maamuzi makubwa na wachezaji kutonitaka.”
Tangu hapo, amekuwa akifanya kwa mafanikio kazi ya uchambuzi wa mpira. “Napenda kutazama na kuzungumza juu ya soka.na unapata bonsai pale unapochambua ukiwa umeshatazama vizuri na kwa umakini, hapo unaweza kwenda nyumbani, ukafunga mlango na kupumzika. Kuwa kocha ni saa 24 kwa siku zote saba za wiki.”
Amekuwa pia akipiga kampeni juu ya kukuza uelewa wa ugonjwa wa saratani ya kibofu kwa wanume weusi. “Mmoja kati ya wanne huipata (saratani ya kibofu), hatari mara mbili kwa wanaume wote. Baba yangu aliipata, lakini sasa ameshafanya matibabu na ni mzima.”
Kwenye mechi ya pili ya fainali za Kombe la Dunia 1990, England walitoka 0-0 na Wadachi ambao timu yao ilijumuisha wachezaji mahiri Ruud Gullit, Marco van Basten na Frank Rijkaard.
Hata hivyo England waliwaazidia Wadachi kinamna, Gascoigne akionesha mamlaka makubwa uwanjani. Likatokea tatizo moja kubwa – Bryan Robson aliumia kiwiko, hivyo kumweka nje katika mashindano hayo. Licha ya kumpoteza Captain Marvel, hali ya hewa ilibadilika.
Vyombo vya habari vilianza kuiunga mkono timu, wachezaji wakapokea vyema. Ikaonekana sasa kuna uwezekano wa kufanya vyema, tena kukawa na msisimko.
Baada ya majeraha ya Robson, Terry Butcher, beki matata wa kati alikuwa nahodha. Anakumbukwa zaidi kwa jinsi alivyokuwa akishangilia suluhu dhidi ya Sweden 1989 akiwa amelowa damu.
Hakuna kinachowakilisha roho yake isiyotawalika, lakini ni mtu mkarimu mwenye kuwajali wengine. “Nawaza juu ya hilo mara kwa mara,” anasema, akikumbukia ya 1990. “Kama leo – tunacheza dhidi ya Ujerumani. Harry Kane anapoiongoza timu, unajiweka kwneye nafasi hiyo kwa sababu umeshakuwa hapo.”
Kipi kilizifanya fainali za 1990 maalumu kwa Butcher ni kwamba zilikuja wakati soka ya England ikiwa kwenye aina ya mkwamo. Baada ya mafanikio ya 1966 na kufika robo fainali 1970, England hawakufuzu kwa fainali za 1974 wala 1978. Walirejeshwa nyumbani 1982 baada ya hatua za makundi bila ya kupoteza hata mechi moja.
Katika fainali za 1986 ilishuhudia kwenye robo fainali Diego Maradona akija na bao la ‘Mkono wa Mungu’. Miaka ya ’70 na ’80 ilikuwa ya jinamizi kwa Timu ya Taifa ya England. “Ilikuwa ngumu kukubali, ukizingatia kwamba sote tulihisi tulikuwa tumesababisha hayo,” Butcher anasema.
“Ilivyo ni kwamba kulikuwapo na marufuku ya klabu za England kwenye mashindano ya soka la Ulaya, zikionekana kukumbatia wahuni.”
1990 ilitoa ishara ya mwanzo mpya: “Italia 90 iliwapa wachezaji nan chi kiburi kwa kiasi kikubwa. Nikihisi: tulirejea tena.”
Baada ya kuacha kucheza, Butcher alifundisha timu 10, kuanzia Coventry City nchini England hadi Timu ya Taifa ya Ufilipino. Alitokea pia kuwa mchambuzi kwenye 5 Live kwa mechi za England, na ilikuwa kichekesho.
“Tunapozungumza, anasubiri zile taa za usiku dimbani Wembley. Nafanya ukarimu, kuzungumza takataka na kulipwa kwa ajili hiyo.”
Anauliza ni nani nitaongea naye baadaye. Mark Wright, nasema. “Na kweli anafanya hivyo, Wrightly. Nampenda sana, ni jamaa mzuri, wote.”
“Unajua, hadi sasa sijatazama tena nusu fainali zile kwenye televisheni,” Mark Wright ananiambia. Kwa nini? “Kwa sababu najua jinsi tulivyokuwa tumekaribia kufika huko (nusu fainali) siwezi kujisumbua kuzitazama. Yaani unafika karibu kiasi hicho cha Kombe la Dunia. Tunajua tulikuwa wazuri kuliko Ujerumani.”
Japokuwa anishi Wirral, kaskazini magharibu mwa England, nakutana naye kwenye klabu ya golf, Derby, sehemu ambayo hupata kinywaji na washirika wake wawili wa biashara. Wright aliyechezea Timu ya Taifa ya England mara 45 hakujua kwamba angepata kuja kuwa mwanasoka wa kulipwa
Alikuwa amejipanga kuwa mwalimu wa PE (elimu ya viungo) na ni mmoja wa wachezaji wachache sana wa kizazi chake aliyebaki shuleni na kusoma A-level. Ni jitu kubwa lenye kutawala kwenye majadiliano.
Wright alikuwa ingizo la kushangaza kwenye timu, akiwa beki wa kati wa tatu, na alianzishwa kwenye mechi dhidi ya Uholanzi. Kulikuwapo uvumi kwamba wachezaji ndio walitoa wito wa mabadiliko, lakini Wright anasema lilikuwa wazo la Bobby Robson.
“Aliniambia baada ya mechi ya kwanza: ‘tunajiandaa kubadilika kuingia kwenye mfumo wa fagia fagia, na nakutaka ufagie.” Wright aliishia kufunga bao la ushindi dhidi ya Misri, lililowapandisha England hadi hatua ya mtoano – bao lake pekee la kimataifa.
Kama asemavyo Butcher, Wright anaweza kuizungumzia England. Anaweza kuelezea kila mechi.
Katika mechi dhidi ya Ubelgiji hatua ya 16 unakuwa na bahati kidogo, kasha Platty anafunga bao zuri la aina yake. Dhidi ya Cameroon (kikosi cha kushangaza kwenye mashindano hayo ambacho England ilikutana nacho kwenye robo gfainali), hawakuwa na cha kupoteza.”
Ajabu, England wakawa nyuma kwa 2-1 wakikabiliana na mshituko wa kutolewa mapema, hadi pale Gary Lineker alipofunga kwa penati kuiokoa siku ya England.
Wright alimaliza mechi ile akiwa amefungwa usoni akiwa pia ameumia zilipo nyusi, baada ya kile kilichoonekana kama kugongana na Roger Milla wa Cameroon.
Leo hii, anakiri kwamba haikuwa hivyo – bali alikosea yeye tu. “Nilimwendea na kugonga jicho langu nyuma ya kichwa chake.” Kwa hiyo ulikuwa unajaribu kumpiga kwa nguvu? Anaachia tabasamu kubwa. “Ilikuwa kufanya uwapo wangu uhisiwe au uonekane. Hivyo ndivyo mechi ilikuwa ikichezwa.”