Menu
in

Fahamu mambo adimu kuelekea fainali UEFA leo

Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

MASHABIKI wa soka nchini Uingereza leo watashuhudia timu zao zikipepetana kwenye mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Si hao pekee bali kote duniani leo kutakuwa na mwelekeo mmoja kujua nani ataibuka bingwa kati ya Chelsea na Manchester City za Uingereza.

Fainali bila makocha wazawa

Tanzania Sports
Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

Kama kuna kitu ambacho inafikirisha katika taifa hili ni namna ambavyo makocha wa kigeni wanavyowakilisha timu za Chelsea na Manchester City. Makocha wote wawili wana sifa kubwa katika kandanda lakini si wazawa wa Uingereza.

Thomas Tuchel ni kocha wa Chelsea. Huyo ni mzaliwa wa Ujerumani, yaani ni zao la ukocha wa soka wa Kijerumani ambaye amepitia katika nchi mbalimbali kabla ya kutua Chelsea. Tuchel alizinoa Mainz na Borussia Dortmund za Ujerumani na baadaye akaelekea kuwanoa matajiri wa PSG.

Akiwa PSG alifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali lakini akaishia kuambulia kilio kweye fainali ya UEFA msimu uliopita baada ya kuchapwa na Bayern Munich nchini Ureno. Desemba mwaka 2020 alifukuzwa kazi PSG, lakini siku chache baadaye akachukuliwa kuinoa Chelsea. Kwa Tuchel akitwaa taji hilo litakuwa la kwanza kwenye ngazi ya Ulaya.

Kwa upande wake Man City wanafundishwa na kocha mwenye mafanikio lukuki, Pep Guadriola. Awali Guardiola alikuwa kocha wa Barcelona ambako alifanikiwa kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya. Baada ya hapo alingatuka katika soka kabla ya kuibukia Bayern Munich katika ligi ya Ujerumani. Akiwa Ujerumani alitwaa mataji mbalimbali lakini alikosa Ligi ya Mabingwa. Pep Guardiola ni raia wa Hispania.

Timu za matajiri wa nje

Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

Kitu kingine adimu katika fainali ya Ligi ya Mbaingwa leo ni umiliki wa timu zote mbili za Man City na Chelsea. Matajiri wanaomiliki Manchester City ni familia ya huko Uarabuni. Hali kadhalika tajiri anayemiliki Chelsea anatoka nchini Urusi akiwa na uraia pia wa Israel, Roman Abramovic. Matajiri wote hao si wazaliwa wa Uingereza.

Kuadimika kwa wachezaji wazawa

Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

Miongoni mwa mambo adimu kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mbaingwa leo ni idadi ndogo ya wachezaji wazawa wa Uingereza katika vikosi vya Chelsea na Man City. Mathalani Chelsea wachezaji wazawa wa Uingereza wenye uwezo wa kupangwa kikosi cha kwanza ni Chilwell na Mason Mount. Katika kikosi cha Man City wenye uhakika wa kuingia ni watatu pekee, winga Raheem Sterling , beki wa kulia Kyler Walker na beki wa kati John Stones. Hilo lina maana katika fainali ya leo wachezaji wa wazawa wa Uingereza watakuwa watano kwenye vikosi vya kwanza.

Ndoto ya matajiri kutawala Ulaya

Moja ya mambo ambayo matajiri wanaomiliki  nyakati hizi ni kushindwa kuhuisha utajiri wao na mafanikio ya klabu katika ngazi ya kimataifa. Wengi wameishia kutawala Ligi za ndani lakini linapofika mashindano ya kimataifa wamekuwa wakifeli hivyo kufukuza makocha wao mara kwa mara.

Wakati Thomas Tuchel anataka kuandika historia yake binafsi kutwaa taji la Ligi ya Mbaingwa Ulaya, naye Pep Guardiola anataka kuweka rekodi yake ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na Manchester City. Baada ya kutamba kwneye EPL, ni wazi sasa Pep ana kibarua cha kuthibitisha uhodari wa timu aliyoijenga ya Man City. Pia Pep anatakiwa kuwapa tabasamu waarabu katika ndoto yao tangu walipoinunua timu hiyo.

Kwa Thomas Tuchel anatakiwa kumwonesha tajiri wake Roman kuwa yeye si mtu wa kubahatisha na amepania kutwaa taji hilo. Pia atawaonesha waarabu wa PSG kuwa walikosea kumfukuza kazi kwani anao uwezo mkubwa wa kunyakua mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa.

Washambuliaji wa asili

Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

Mfungaji bora wa Manchester City katika Ligi Kuu England msimu huu ni Ilkay Gündogan akiwa ametupia wavuni jumla ya mabao 13. Jorginho ni kinara wa mabao kwa upande wa Chelsea akiwa ametumbukiza wavuni mabao saba, akifuatiwa na Tammy Abraham, Mason Mount na Timo Werner ambao kila mmoja amepachika mabao 6. Naam, timu hizo zinatarajiwa kukutana katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa leo Jumamosi.

Man City na Chelsea zote zinatumia viungo wao kama washambuliaji hivyo kucheza bila mshambuliaji kamili kutokana na sababu mbalimbali.  Tuchel anaonekana hatumii mshambuliaji wa asili kwenye kikosi chake ingawa Timo Werner na Kai Havertz wamepangwa kucheza safu ya ushambuliaji, na pengine Werner ni mshambuliaji kamili hivyo huwezi kumchezesha kama Kai Havertz. Kwa Pep Guadiola anaweza kuwapanga Bernando Silva, Kevin De Bruyne na Mahrez.

https://goalballlive.com/list-of-african-players-that-have-won-the-champions-league/

Ni fainali ya akina Mendy

Kuna Eduardo Mendy, ambaye ni golikipa namba moja wa Chelsea, halafu kuna Benjamin Mendy mwingine ambaye ni beki wa kushoto wa Manchester City. Hilo lina maana katika fainali ya UEFA leo kuna mwanafamilia mmoja atanyakua taji hilo ni Mendy wa Chelsea au Man City.

Mtanange wa Wabrazil

Kwenye fainali ya leo kuna wachezaji ambao ni raia wa Brazil. Kila msimu wachezaji wa Brazil huwa wanakuwepo kwenye vikosi vya timu. Chelsea wanaye beki kisiki Thiago Silva ambaye ni nahodha wa Brazil na mwenzake Jorginho, watapepetana na Wabrazil wenzao wa Man City, golikipa namba moja Eduardo na kioungo mkabaji Fernandinho.

Mastaa wa Afrika wameadimika UEFA leo

Katika vikosi vya leo mastaa wa kutoka Afrika ni wachache kuliko miaka ya nyuma ambapo wengi walitawala vikosi vya timu za ulaya. Chelsea wanaye Eduardo Mendy ambaye ni raia wa Senegal, wakati Man City wanaye Riyad Mahrez ambaye ni nyota kutoka Algeria. Angalau hawa wanawakilisha vipaji vya bara la Afrika ambalo limekuwa likitoa nyota kadhaa kwenye michezo ya fainali kama hii ya leo.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version