Menu
in

Eymael Aponda Usajili Yanga

Eymael

Eymael

Baada ya kuachana na Yanga kwa kashfa ya udhalilishaji wa ubaguzi wa rangi Mbeligiji Luc Aymael, aponda maamuzi ya timu ya Yanga katika dirisha la usajili linaloendelea.

Aymael ameongea na moja ya vyombo vya habari hapa nchini amesema kuwa kuna baadhi ya nyota walitakiwa kubaki ili kuzidi kuipiganania timu kama walivyo fanya msimu uliopita.

imeonesha wazi katika maelezo yake kuwa maamuzi ya kumuacha  aliyekuwa mfungaji bora wa Yanga David Molinga ‘Falcao’ hayakuwa mazuri kwa upande wake.

Huku akiwapigia chapuo baaadhi ya wachezaji ambao wamekatwa katika wale 16 waliotangazwa.

Yeye ameona wazi kuwa katika wachezaji walioachwa kuitumikia Yanga ambao pia walikuwepo msimu uliopita walistahili kubaki na baadhi ya waliobaki ndio haswa walitakiwa watoke.

Yanga walipitisha panga la nyota 16 msimu huu na kuingiza wengine ndani ya timu yao.

Sasa Aymael ambaye amefungiwa miaka miwili na Shirikisho la Soka la Tanzania kwa utovu wa nidhamu amejinadi kuwa sio rahisi kupangua maamuzi ya mtu ila kama angebaki Yanga yasingetokea haya ambayo yanayoendelea.

Yanga imekuwa ikikosolewa kwa maamuzi yake ya kuachana na baadhi ya wachezaji waliofanya vizuri msimu huu kama vile; David Molinga ‘Falcao’, Patrick Sibomana, Juma Abdul na Kelvin Yondani.

Maneno ya Aymael juu ya kuondoka kwa baadhi ya nyota ni haya yafuatayo.

“Nimepata taarifa kuwa Yanga wameachana na wachezaji 16, nisingependa kuliongelea sana suala hili lakini kwa mtazamo wangu nadhani maamuzi haya hayapo sahihi kwa asilimia zote.

“Kama ningesalia kuwa kocha wa kikosi basi naamini ningekuwa na mawazo tofauti kwani ningeendelea kubaki na baadhi ya wachezaji walioachwa na kuwaondoa waliopo kikosini hivi sasa.

“Tayari nimeongea na Molinga kuhusiana na suala hili lakini kama ambavyo nimesema siwezi kuingilia sana maamuzi ya watu wengine,” alisema Eymael.

Hadi sasa usajili unaendelea na tetesi zinazoibuka kuwa Yanga inaweza kupata nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Afrika inazidi kupamba moto mara baada ya Libya kufungiwa mwaka mmoja.

Wachezaji ambao tayari wametambulishwa na Yanga ni pamoja na Bakari Nondo Mwamnyeto beki wa kati ambapo ataungana na Lamine  Moro na Said Makapu huku Abdallah Shaibu ‘Ninja’ naye akisajiliwa katika beki ya kati.

Wengine ni Mustapha Yassini beki wa kushoto akisaidiana na Adeyun Saleh huku upande wa kulia akisajiliwa Kibwana Shomari kutoka Mitbwa Sugar akiziba pengo la Juma Abdul.

Sehemu ya kiungo ya ukabaji amesajiliwa Zawadi Mauya akiziba nafasi ya Papy Tshishimbi ambaye anatajwa kutakiwa na AS Vita ya nchini kwao Kongo.

Winga ya kushoto tayari amesajiliwa Farid Mussa aliyekuwa huru baada ya kutoka Tenerife CD ya nchini Hispania.

Waziri Junior aliyekuwa mshambuliaji wa Mbao FC kajiunga na Yanga katika kusuka timu yao.

Katika eneo la ushambuliaji amesajiliwa Yacouba Sogne akitokea Medeama FC ya nchini Ghana.

wachezaji wanaotajwa kusajiliwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa ni pamoja na Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda ambapo dili la mshambuliaji huyu kama lina yumba hivi.

Wengine wanaohusishwa ni pamoja na Heritier Makambo aliyewahi kuichezea Yanga, Shiboub wa Simba na Deo Kanda.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version