Menu
in , ,

Eric Ten Hag aliidharau Man United

Klabu ya Manchester United ya England imetangaza kumfukuza kazi kocha wake Eric Ten Hag na nafasi yake kuchukuliwa na staa wao wa zamani Ruud Van Nistelrooy. Uamuzi wa Manchester United umetokana na kushuhudia klabu hiyo ikizabwa mbele ya wakongwe wa EPL West Ham. Klabu hiyo kwa miaka karibu kumi imekuwa ikiishi katika maisha ya ajabu sana kwani vipigo kwao lilikuwa jambo la kawaida. Lakini yapo mambo ambayo yameonesha wazi kocha huyo alikuwa anaidharau timu hiyo.

Kukosa viwango vya UCL

Hakuna kauli mbaya ambayo inaweza kuathiri taasisi kama mkuu wake anatoa matamshi ambayo yanaashiria kuanguka au kushindwa kufanya kazi sababu ya wafanyakazi duni. Kauli kama hiyo ilikuwa na maana kocha mkuu mwenye jukumu la kushauriana na menejeimenti ameshindwa kazi ya kupendekeza au kusajili wachezaji muhimu na wenye thamani kwenye klabu hiyo. Ten Hag alionesha kushindwa vibaya pale aliposemma Manchester United haikuwa tayari kuchuana kwneye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Tanzania Sports
Mpasuko wa mahusiano ndani ya Man U

Kauli yake iliashiria kama vile Manchester United ni timu ndogo ambayo haiwezi kuwa nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa. Akiwa kocha aliwajibika kufundisha mbinu zote na kuifanya Man United inarudisha ubora wake kwenye mashindano makubwa. Kimsingi kauli yake iliashiria kana kwamba alikuwa anafundisha timu inayopigania kushika daraja.

Ugomvi na Ronaldo

Kabla ya kuondoka Manchester United, Cristiano Ronaldo aliyerudi klabuni hapo akiutokea Juventus Turin alibainisha wazi timu hiyo ilipoteza ile thamani ya zamani. Ronaldo alilalamikia karibu kila kitu, mbinu za kocha, vifaa vya mazoezi,uendeshaji wa timu kwa ujumla wake. 

Ronaldo alikasirishwa na uamuzi wa kocha Eric Ten Hag kutaka kumwingiza uwanjani katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs wakati zikiwa zimebaki dakika 3 kumalizika kwa mchezo. Ronaldo alihisi ni ukosefu wa heshima kumpa dakika tatu kucheza dhidi ya Spurs. Jambo hili lilileta vurumai kati ya Ronaldo na uongozi wa Manchester United na kuamua kuachana kwa amani. Ronaldo alisema haiwezekani Man United iwe katika hali ya kushindwa kuwasikilzia  waandamizi wanaoijua klabu hiyo kuliko Ten Hag. 

Vuta yake na Sancho

Jadon Sancho ana kipaji kizuri sana. ni sababu hiyo Manchester United ililazimika kumng’oa Dortmund na kumleta Old Traford. Hata hivyo Eric Ten Hag alifanya kosa kubwa kummkoa mchezaji wake kwenye mahojiano na vyombo vya habari ambayo kufanyika mara baada ya mchezo. Kuona hivyo Jadon Sancho naye akatumia mtandao wa kijamii kueleza umma kuwa wasiamini kila wanahcoambiwa. 

Sancho alikataa kuomba radhi kwa kile alichokiita ni sawa na kukubaliana na maneno ya kocha wake. Man United ikalazimika kumrudisha Dortmund kw amkopo ambako alicheza hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata msimu ulipomalizika Sancho hakuwa na maisha tena Old Traford hivyo akaondolewa kupelekwa kwa mkopo wa msimu mzima. Ugomvi huu uliathiri mwenendo wa kocha huyo na kusababisha mgawanyiko kwenye timu.

Viwango kushuka

Jambo ajabu ni kwmaba wachezaji wengi wa Man United wameonekana kushuka viwango na hawana ongezeko la maarifa. Aliyekuwa kocha msaidizi wa Manchester United, Benny McCathy alipata kusema “ni ajabu sana kwa kile kinachoonekana kwenye kiwanja cha mazoezi, lakini hakionekani kwenye siku ya mchezo. Unabaki kujiuliza ni nini kinachotokea kwa wachezaji,” kocha huyo raia wa Afrika kusini alifanya mahojiano na vyombo vya habari vya Ureno na Afrika kusini akishangazwa na hali ya viwango vya wachezaji wa Man United mazoezini na siku ya mchezo. 

Baadhi ya wachezaji wanaonekana dhahiri hawana ongezeko la viwango chini ya Eric Ten Hag. Marcus Rashford mshambuliaji aliyetajika kutamba amekuwa nyanya na haonekani kuwa kwenye maarifa mapya ya kukuza kiwango chako. Ni sababu hiyo hata aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa England, Gareth Southgate aliamua kumtosa kwenye kikosi chake cha mashindano ya Euro.

Mataji madogo

Kati ya mambo ambayo yaliidharaulisha Man United ni kujivunia kocha anayetamba kwa kutwaa mataji mawili ndani ya miaka miwili. Yaani Manchester United ilifikia hali ya kuamini kuwa taji la FA lilikuwa ndicho kigezo cha kumbakiza Ten Hag katika timu yao. Ukame wa mataji kwa Man United ni ishara ya mambo kwenda ovyo hivyo  uongozi ulipaswa kuona aibu kukumbatia kocha anayejivunia mataji madogo.

Bila shaka yoyote ilifika mahali Man United kufungwa kikawa kitu cha kawaida., sifa za Man United zikawa zinaporomoka kila kukicha kwa sababu kocha wao aliidharau timu yake, lakini viongozi wake walichalewa kuchukua hatua za kumwondoa na kuajiri mwingine.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version