Ligi Kuu ya England (EPL) imeanza kushika kasi na kwa wikiendi iliyopita yapo kadhaa ya kuzungumzia, yenye alama chanya na hasi.
La kwanza ni Manchester United ambao licha ya kushinda dhidi ya Brighton, wachezaji wake walionekana wazi kwamba miili yao ilikuwa imechoka. Kama kawaida, kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba wanajijenga na watakuwa sawa.
Solskjaer anasema kwamba wanahitaji wiki tatu au nne kwenda sawa na timu nyingine ‘kubwa’ za EPL. Wana alama tatu walizopata kwa mbinde baada ya mechi mbili, wachezaki wakikosa ile kasi ya mchezo inayotakiwa kwa wakati ambao hawakuwa na maandalizi ya kiwango kikubwa kwa msimu huu wa 2020/2021.
Ajabu ni kwamba, Kocha wa Timu ya Taifa ya England – Three Lions, Gareth Southgate, anasema kwamba Septemba hii katika kikosi chake, wachezaji walioendelea na mechi za Ulaya ndio walikuwa timamu zaidi uwanjani kuliko wale waliopumzika.
Solskjær ana maoni tofauti, akisema wachezaji wanachoka. Anasema miili hiyo inahitaji kupumzika, hivyo itawachukua muda kurudi kule juu katika msimamo wa ligi kutoka wkwenye nafasi ya 13 waliyomo. Walishinda kwa shida 3-2 wakiwa ugenini na kupata alama tatu.
Everton wanaonolewa na mkongwe Carlo Ancelotti, kwa upande mwingine, walifanikiwa kupata ushindi wa tatu – ikiwa ni kwa mechi zao zote na kuongoza ligi, hata kama itakuwa kwa muda mfupi. Amefanya matumizi mazuri ya wachezaji wake kujihakikishia ushindi.
Manchester City walitiwa adabu na Leicester baadda ya kubamizwa mabao 4-1 katika mchezo ambao City walionekana wazi hawakuwa timamu. Riyad Mahrez akicheza dhidi ya timu yake ya zamani, alionekana kutokuwa mzuri.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola anaweza kusema kwamba hakuwa na wachezaji wake muhimu kadhaa, lakini kadhia aliyopata ni kubwa na hakika haikutarajiwa. Katika uwanja mtupu, Mahrez alivyofunga bao dhidi ya klabu alioshiriki kuwapa ubingwa 2015.
Guardiola alionekana kukosa mbinu mbadala, kwani wachezaji kama Leroy Sané na David Silva walishaondoka, huku akimkosa Bernardo Silva aliyeumia huku Raheem Sterling akicheza kama mshambuliaji wa kati kutokana na kukosekana kwa Sergio Agüero na Gabriel Jesus.
Matokeo mengine yalikuwa Crystal Palace kulala nyumbani 1-2 dhidi ya Everton; Chelsea kulazimishwa sare ya 3-3 na West Bromwich Albion na Burnley wakiwa nyumbani wakipoteza kwa Southampton kwa 0-1.
Timu ambazo hazijapata alama katika mechi zao mbili ni Burnley, Fulham, Sheffield United na West Ham.