Menu
in , , ,

England vs Croatia, France vs Belgium

England vs Croatia
Ufaransa vs Ubelgiji

Mambo yalikuwa si ya kawaida nchini Urusi Jumamosi ya jana, baada ya
mechi mbili kali za robo fainali ya Kombe la Dunia, ambapo England na
Croatia wameunganana Ufaransa na Ubelgiji kufika nusu fainali.

Ijumaa ilishuhudia Ufaransa wakicheza kufa na kupona kuwatoa Uruguay
waliokuwa wakiogopewa sana, lakini Ufaransa wakafanikiwa kuwachakaza
2-0 kupitia kwa Raphael Varane na Antoine Griezman. Ilikuwa mechi
ambayo mshambuliaji mahiri wa Uruguay, Edinson Cavani hakucheza baada
ya kuumia kwenye mechi ya 16 bora.

Ilikuwa ni siku ambayo vigogo wengine wa soka, Brazil, walioneshwa pa
kutokea na Ubelgiji baada ya kuchapwa 2-1, Neymar akisema ameumia sana
na itakuwa vigumu kwake kurudi kwenye soka ya ngazi ya klabu.


England walisababisha sherehe kubwa kona mbalimbali za England lakini

pia huko nchini Urusi hadi baadhi ya wachezaji wakashangilia na
familia zao, kama ilivyokuwa kwa Jesse Lingard wa Manchester United
aliyesherehekea, kukumbatiana na kupiga picha na mamaye mzazi.

Ilikuwa baada ya England kufanikiwa kuwazidi nguvu wabishi Sweden,
tena kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Harry Maguire na Dele Alli na
kuweka historia mpya kwa England kufika hatua ya nusu fainali kwa mara
ya kwanza tangu 1990 Italia, yote yakiwa ni mabao ya vichwa katika
mechi iliyofanyika Samara.

Katika mechi ya pili ya robo fainali kwa Jumamosi hiyo, Urusi
walichuana vikali na Croatia, wakiongoza bao lililokuja kusawazishwa
na kwenda dakika 30 za ziada, Croatia wakaongoza lakini Urusi
wakachomoa, ubishi ukamalizwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati
ambapo Croatia walishinda kwa 4-3 na kukatiza chereko za wenyeji.

Kwa matokeo hayo ya robo fainali, Ufaransa watapepetana na Ubelgiji
Jumanne hii saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki, wakati England
watakuwa na kibarua dhidi ya Croatia siku inayofuata, ikimaanisha sasa
ni timu nne tu zinabaki Urusi, wengine wakiwa wameshafika nyumbani na
baadhi wapo njiani.

Gareth Southgate, kocha wa England, alichagua kikosi cha chipukizi
wengi na katika kuwapanga hakuwa akidhaniwa angepata matokeo mazuri
kiasi hiki, lakini sasa amethibitisha ubora wake. Chama cha Soka cha
England (FA) kinaamini atabaki na timu hadi mkataba wake umalizike,
licha ya kwamba ni wazi atakuwa anatakiwa na timu nyingine, iwe za
taifa au klabu.

Kati ya wachezai walioonesha umahiri ni golikipa wa Everton, Jordan
Pickford ambaye amesifiwa na yule wa Chelsea anayechezea Timu ya Taifa
ya Ubelgiji, Thibaut Courtois. Three Lions, kama wanavyojulikana timu
ya taifa ya England walitwa ubingwa huo 1966 walipokuwa wenyeji,
lakini wakapoteza kwa mikwaju ya penati kwa Ujerumani Magharibi 1990.

Lakini kwa jinsi fainali za mwaka huu zilivyo na maajabu, inamaanisha
kwamba wanakabiliana na timu inayoshika nafasi ya 20 kwa kiwango cha
soka, kutafuta kucheza fainali dhidi ya Ubelgiji au Ufaransa.

Wakati hayo yakijiri, mataifa mbalimbali yameanza kujua hatima ya
makocha wao, ambapo wakati Joachim Low ataendelea kuwafunza Ujerumani
licha ya kutolewa kwenye hatua ya kwanza, yule wa Hispania, Fernando
Hierro, aliyepewa timu siku mbili kabla ya mashindano kuanza ameachia
ngazi.

Hierro ameamua kuondoka na wala hatarudi kwenye kazi yake ya awali ya
ukurugenzi wa michezo. Alipewa kazi hiyo kwa muda baada ya chama cha
soka cha huko kumfuta kazi Julen Lopetegui kwa hatua yake ya kuamua
kujiunga na Real Madrid. Hispania walitolewa kwa penati na Urusi
kwenye hatua ya 16 bora.

Hierro, 50, amesema ameamua kutafuta kazi sehemu nyingine. Mtangulizi
wake, Lopetegui alichukua ukocha huo 2016 baada ya kustaafu kwa
Vicente del Bosque na tangu ajiunge huko hakupata kupoteza mechi hata
moja.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version