in , , ,

England nje Euro ya Vijana

Ndoto za England kufanya vyema kwenye michuano ya vijana ya Euro zimefutika baada ya kucharazwa 3-1 na Italia kwenye dimba la Ander nchini Jamhuri ya Czech.

Kwa matokeo kwenye mechi nyingine ya Kundi B kuwa Ureno kutoshana nguvu na Sweden, vijana wa Gareth Southgate hawakuwa na cha kupata zaidi ya kutolewa kwenye mashindano hayo.

England walikuwa wakihitaji pointi moja tu kuvuka hatua hii ya makundi, lakini ilikuwa shida kubwa kuipata, kwani katika nusu saa ya kwanza walishalala 2-0 na hadi mpira ukikaribia kumalizika walikuwa nyuma kwa 3-1.

Waliruhusu mabao mawili ndani ya dakika mbili tu – yakifungwa na Andrea Belotti na Marco Benassi kunako dakika ya 24 na 27 ya mchezo. Benassi aliwaadhibu England kwa kutia la pili kwa kichwa dakika ya 72 hivyo bao la Nathan Redmond la dakika ya 90 halikusaidia kitu kwani England wameondoka wakishika mkia wkenye kundi lao.

Sasa wachambuzi wa soka wataangalia sababu na athari za kuwaondosha kikosini wachezaji waliokuwa wanafuzu kuwamo kama Raheem Sterling, Ross Barkley, Luke Shaw na Alex Oxlade-Chamberlain.

Kocha Southgate aliyekuwa kwenye kikosi cha England kilichofuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 1998 kwa suluhu dhidi ya Italia, ameeleza nia yake ya kubaki kocha wa kikosi hicho licha ya matokeo mabaya.

Vijana hawa wa England walifuzu kwa mashindano haya kwa kupoteza pointi mbili tu kwenye zile za kufuzu lakini wakaonekana kukosa ufanisi wakati ulipotakiwa. Licha ya kuwapo mshambuliaji anayesifiwa sana wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, hapakuwapo matumaini yoyote ya kuokoa jahazi la samba hao wadogo.

Alikosa nafasi nzuri ya kufunga sambamba na mwenzake, Danny Ings, ambapo Italia walikuwa wazuri katika kujilinda na England wakizorota kwenye utoaji pasi.

Hii ni mara ya tatu mfululizo England wanashindwa kuvuka hatua ya makundi kwa U-21 na kocha wao amesema kwamba kazi inaendelea nyuma ya pazia kubaini kisa cha wachezaji kushindwa kucheza aina ya soka ambayo ingeoneshwa na kikosi cha kwanza.

Amesema kwa kuwa mkataba wake unakwenda hadi 2017 angependa kuendelea kuwanoa vijana hao. Akizungumzia kutolewa kwao, nahodha wa zamani wa England, Alan Shearer amesema ikiwa hayo ndiyo maendeleo ya soka, anazidi kushangazwa na kuogofishwa.

Nahodha mwingine wa zamani wa England, Michael Owen amesema inauma sana kuona kwamba vijana wanatakiwa kurudi tena darasani kujifunza jinsi ya kucheza soka baada ya kutoa matumaini makubwa awali.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

26 WAITWA TAIFA STARS

Real Madrid wamtaka Koscielny