El Clasico mikononi mwa Munuera
nani kucheka au kununa?
Jumamosi ya wiki hii dunia nzima itaelekeza macho na masikio katika uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona kati ya miamba miwili ya soka nchini Hispania. Barcelona watakuwa na staa wao Lionel Messi akiwa anaingia msimu wa tatu bila mshindani wake wa karibu Cristiano Ronaldo.
Huo utakuwa mchezo wa 7 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Hispania msimu huu 2020/2021. Huku timu zote zikiwa na mwelekeo wa kutaka kuibuka washindi wa Ligi hiyo mwishoni.
Real Madrid itaingia uwanjani ikiwa imejeruhiwa mara mbili; kwanza ilifungwa kwenye mchezo wa mwisho wa La Liga dhidi ya Cadiz. Pili imezabwa mabaom3-2 dhidi ya Shakhtah Donesk kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Barxcelona wataingia uwanjani wakiwa na kocha mpya Ronald Koeman, huku Madrid wakiendelea kutegemea ‘uchawi’ wa Zinedine Zidane, ambaye pia ni bingwa mtetezi wa Ligi hiyo.
EL CLASICO BILA SHANGWE
Mchezo huu ni kama ‘derby’ ya Ligi yoyote ile. Ni kama Olrando Pirates na Mamelodi Sundowns au Kaizer Chiefs. Ni kama Yanga na Simba, AC Milan na Inter Milan. Ni pambano la wapinzani wa jadi ambao wanataka kutangaza zaidi ufalme wao.
Katika pambano hili mashabiki wakiwa wameketi kwenye viti au masofa yao yao nyumbani watashuhudia pambano la kwanza la wapinzani wa jadi bila kujazana uwanjani. Pambano hili linakwenda kuweka historia kuwa El Clasico ambayo mashabiki hawakuruhusiwa kuingia uwanjani.
Sababu inakuwa ni moja tu; kuepuka kuambukizana zaidi ugonjwa corona. Si mashabiki wa wenyeji wa Barcelona wala wageni Real Madrid. Hakuna mauzo ya tiketi kwa vle hawaruhusiwi kuingia uwnajani. Hakuna mauzo ya vinywaji uwanjani. Hakuna amsha amsha uwanjani. Hakuna zomea zomea uwanjani. Vtote hivi vinakosekana sabababu ya corona.
Katika pambano hilo kila upande utakuwa na hamu ya kushinda. Ronald Koeman atataka kuwadhihirishia mabosi wake wa Barcelona yu kocha sahihi kuokoa jahazi la klabu hiyo ambalo linadidimia siku hadi siku.
Kwa upande wake Zinedine Zidane atataka kuweka rekodi ya kutofungwa kwenye uwanja wa Camp Nou. Zidane hajawahi kufungwa ndani ya dimba hilo tangu awe kocha wa Real Madrid kwa awamu zote mbili. Je makocha hao watamudu kutambiana? Majibu yatapatikana baada ya mchezo.
FILIMBI YA MUNUERA
Kwenye mchezo wa El Clasico, mtu mmoja atakuwa ameshika filimbi katikati ya dimba akichezesha mechi hiyo kwa dakika zote 90. Mtu huyo ni Martinez Munuera. Chama cha soka cha Hispania, RFEF kimetanagza kuwa Munuera ndiye atachezesha mechi ya El Clasico.
Wakati Munuera akishika filimbi kwenye pambano hilo, ndani ya chumba cha VAR atakuwapo mwamuzi mwingine Martinez Munuera
Munuera amechezesha mechi 24 za Real Madrid tangu alipoanza kazi ya uamuzi La Liga. Kati ya mechi hizo imeshinda mechi 15, kutoka sare mechi 8 na imeambulia vipigo katika mechi 4. Mchezo wake wa mwisho kwa Real Madrid ulikuwa walipopambana na Real Sociedad msimu huu.
Aidha, Munuera amechezesha mechi 21 za Barcelona dhidi ya timu mbalimbali. kati ya mechi hizo Barcelona imeshinda mara 15 sawa na Real Madrid. Barcelona wenyewe wametoka sare mechi 3 na kuambulia vipigo katika mechi 3. Mchezo wake wa mwisho kuwaamua Barcelona ulikuwa msimu uliopita walipocheza dhidi ya Leganes na kushinda mabao 2-0.
Katika mechi za Real Madrid amewapa kadi za njano wachezaji watano, wakati Jesus Vallejo peke yake alilimwa kadi nyekundu. Hivyo ni refa ambayo ni mkali kwa wachezaji na inawalazimu kuwa waangalifu mara mbili ya hali ya kawaida.
Munuera kwa sasa ana umri wa miaka 38. Amechagyliwa kuchezesha mechi ya El Clasico kutokana na kiwango bora alichoonesha msimu huu. Uchezeshaji ambao uko mbali na malalamiko, usahihi wa kutafsiri sheria na kuwa karibu kila mahali ambako makosa hufanywa na wachezaji.
Kwa maana hiyo msimu huu Munuera anaweka rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza kuchezesha El Clasico ikiwa tupu. Ni El Clasico isiyo na mashabiki uwanjani. Huenda hii itakuwa histoia yake ya kusimulia wajukuu miaka ijayo.
Na zaidi ni ndiye mwamuzi atakayetajwa miaka ijayo kuwa alichezesha mechi isiyo na mashabiki kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa corona. Ni corona itamweka kwenye ramani, lakini uamuzi bora ndiyo utakuwa na thamani kubwa.
Kwenye pambano hili timu zote zinaingia zikiwa na mapungufu kadhaa. Zote zimekuwa na viwango dumu katika mechi za karibuni. Zote zinajaribu kujijenga zaidi. Barca wamemuuza mshambuliaji wao Luis Suarez, wakati Real Madrid haijasajili mchezaji yeyote.
Hii ni mechi ya kuoneshana umwamba na kutafuta ufalme. Ni nani ataibuka mshindi kati ya kocha mpya wa Barcelona au Zidane kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa Camp Nou? Majibu yatakuja baada ya mechi.