Menu
in ,

Dua la Togo lafika

*Mwamuzi awaminya lakini wafuzu

*Algeria na Tunisia warudi makwao

Togo wameingia robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza.

Chini ya unahodha wa mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Emmanuel Adebayor, Togo walitoka sare ya bao 1-1 na Tunisia, hivyo kusonga kwa uwiano mzuri wa mabao.

Togo wameungaa na Ivory Coast katika kundi D kuingia hatua ya nane bora, ambapo Ivory Coast Jumatano hii wametoka sare ya mabao 2-2 na Algeria.

Licha ya kuonewa na mwamuzi, Daniel Bennett aliyewapa Tunisia penati mbili tata na kuwanyima Togo iliyokuwa ya wazi, Chiriku hao wa Afrika Magharibi walisikiwa dua yao.

Togo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa

Serge Gakpe, bao ambalo wachambuzi walidai mfungaji alikuwa ameotea, Togo wakasawazisha kwa penati.

Tunisia ilihitaji ushindi ili ifuzu kutokana na uwiano wake mbaya wa mabao, hivyo walicheza kufa na kupona, huku wakielekea kubebwa na mwamuzi kupata ushindi waliohitaji.

Hata hivyo, penati waliyonyimwa Togo ilitokana na Adebayor kuzidisha madoido akiwa katika nafasi ya kufunga, akaendeleza chenga za maudhi, hatimaye akaangushwa, ikiwa ni penati dhahidi, lakini mwamuzi alikataa kutoa.

Dakika chache baadaye, mchezaji wa Togo alimkanyaga kwa bahati mbaya wakati wote wakikimbilia mpira, na mwamuzi akatoa penati.

Ilichukua muda kupigwa, kwani wachezaji wa Togo walipinga, ikiwa ni pamoja na kufikia kudondosha kadi ya njano ya mwamuzi, na baadhi yao walionywa kwayo.

Kadiri mchezo ulivyoelekea dakika za mwisho, Togo walicheza kwa kujihami zaidi, na Tunisia wakawa wakitafuta bao muhimu ili waungane na Ivory Coast, lakini haikuwezekana hadi mwisho.

Ivory Coast wakicheza wakijua wameshafuzu, hawakuweka kasi kubwa, huku Algeria waliokwishatolewa wakitafuta kupata heshima.

Algeria walikosa penati katika kipindi cha kwanza, iliyopigwa na Ryad Boudebouz, lakini Sofiane Feghouli alifunga nyingine dakika ya 64, ukiwa ni mpira wake wa kwanza kugusa tangu aingie uwanjani.

Alikuwa ni Feghouli tea aliyempasia Hilal Soudani na kuzitikisa nyavu za Ivory Coast, hivyo kufanya ubao wa matokeo katika dakika ya 70 kusomeka 2-0.

Didier Drogba aliamsha ari ya ushindi kwa Ivory Coast kwa kufunga bao katika dakika ya 77 kabla ya

Wilfried Bony kusawazisha na kuwafanya Tembo hao wamalize mechi za awali pasipo kufungwa hata moja.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version