Kapiga tatu…
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ameanza vyema msimu katika klabu mpya ya Montreal Impact kwa kufunga mabao matatu kwenye Major League Socce.
Kwa hat-trick hiyo, Drogba (37) aliwezesha timu yake kuwafunga Chicago Fire 4-3. Alikuwa ni mshambuliaji huyo mstaafu wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast aliyewasukuma Montreal kwa kufunga mabao muhimu, likiwamo la kusawazisha kwenye kipindi cha kwanza na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 3-3.
Baadaye alifunga bao zuri kwa kichwa, na kudhihirishia ulimwengu wa soka kwamba bado yupo timamu kimwili na kwenye kiwango kizuri. Aliachwa na Chelsea, ikidhaniwa kwamba angepewa kazi nyingine klabuni hapo, lakini akasema angependa kucheza walau msimu mmoja au miwili tena kabla ya kustaafu.
Drogba anaongoza katika timu yao ya taifa kihistoria kwa kufunga mabao 65 kwenye mechi 105 alizochezea. Alihamia Montreal Julai mwaka huu. Kuondoka kwake Chelsea kulikuwa sambamba na kipa wao mkongwe, Petr Cech aliyejiunga na wapinzani wao wa London, Arsenal.
Drogba aliwakumbusha Chicago Fire na klabu nyingine za MLS kwamba bado kuna mabao mengi amebakiza kufunga, licha ya kwamba miguu yake yaweza kuwa imechoka, kwa mshambuliaji kucheza hadi kuvuka umri wa miaka 37.
Ushindi wa Montreal ni wa kwanz akatika mechi tano zilizopita, ambapo walipata kwenda mechi sita mfululizo bila ushindi kwenye mashindano yote na hapo walimfukuza kocha wao, Frank Klopas. Msimu huu umebakiwa