Menu
in

Dk. Jakaya M. Kikwete , awakaribisha ikulu viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF).

Leo asubuhi Mhe. Dk. Jakaya M. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwakaribisha ikulu viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF).

Viongozi wa TBF waliokuwepo ni Musa Mziya Rais wa TBF, Phares Magesa Makamu Rais wa TBF, Michael Maluwe Katibu Msaidizi wa TBF na Marry Mmbaga Mhazini wa TBF, pia alikuwepo ndugu Matoke Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo.

Makamu wa Rais wa TBF ndugu Phares Magesa kwa niaba ya TBF na kwa niaba ya Kocha Greg Brittenham alitoa maelezo mafupi na kumkabibidhi Rais Kikwete Jersey rasmi ya timu ya New York Knicks yenye jina la KIKWETE ambayo ilitolewa na Kocha Greg ambaye alikuwa nchini kuendesha mafunzo ya kikapu kwa vijana nchini ya miaka 17 yaliyofanyika Arusha 9-10 Juni, 2012 na kushirikisha vijana 100 kati yao wa kike 30 na wa kiume 70. Pia ndugu Magesa alimkabidhi Mhe. Rais Jacket maalumu la viongozi wa michezo kutoka chuo Kikuu cha Wake Forest ambako Kocha Greg kwa sasa ni Mkurugenzi wa michezo, kabla ya kuijunga na chuo hiki Kocha Greg alikuwa ni kocha Msaidizi wa New York Knicks kwa miaka 20 na ni moja ya makocha bora sana na wa daraja wa juu kabisa duniani wa kikapu katika Strenth and Conditioning.

Pia Rais wa TBF Mziya amkabidhi Mhe. Rais Kikwete Mpira wa kikapu toka kwa wadau wa TBF Kampuni ya Coca Cola kupitia kinywaji cha SPRITE.

Mhe. Rais alishukuru TBF, Kocha Greg , Timu ya New York Knicks, Chuo Kikuu Cha Wake Forest na Coca Cola kwa vifaa hivyo vya michezo na akaomba tuimarishe mahusiano nao ili kuinua mchezo wa kikapu nchini.

Mhe. Kikwete pia alisema atakapo safiri kwenda Marekani katika safari za kikazi atajitahidi kuwasiliana na timu hii ya New York Knicks na wadau wengine ili awashukuru na kuwaomba waendelee kushirikana nasi katika maendeleo ya mchezo wa kikapu nchini.

Katika mazungumzo hayo kati ya Rais Kikwete na Viongozi wa TBF, Rais wa TBF Mizya alimueleza Mhe. Kikwete mipango na majukumu yanayokiabili TBF kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuandaa Kombe la Taifa mwezi Oktoba 2012 yatakayofanyika Tanga na Mashindano ya timu za Taifa kanda ya 5 ya FIBA mwezi Desemba yatakayofanyika Dar Es Salaam, mpiango mingine ni kuendelea kuendesha mafunzo ya vijana wadogo, kufundisha makocha na waamuzi zaidi ili kuinua mchezo kuifundi na uendelelezaji wa viwanja vya michezo kwa kushirikana na wadau wetu.

Pia katika kikao hicho cha leo TBF iliwasilisha maombi kwa Serikali ili itoe kipaumbele katika awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa Taifa kwa kujenga uwanja mkubwa michezo wa ndani na pia TBF ilimuomba Mhe. Rais aangalie uwezekano wa kusiadia gharama za kupata walimu wa kikapu toka nje. TBF ilimweleza Mhe. Rais kuwa kwa sasa tayari imeshafanya mawasiliano na makocha kadhaa wa ngazi ya juu toka Marekani na muda wowote mazungumzo yakikamilika watapelekea taarifa rasmi serikalini kwa hatua zinazofuata. Kimsingi Mhe. Rais Kikwete alisema Serikali itafanyia kazi maombi ya TBF ila alishauri Makocha hawa toka nje walenge zaidi kufundisha makocha wetu wa ndani na TBF ilikubaliana na ushauri wa Mhe. Kikwete.

TBF ilimueleza Mhe. Kikwete mipango na malengo yake ikiwa ni kucheza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil na Mhe Rais akashauri tujitahidi kwanza tuhakikishe tunachukua ubingwa wa kanda ya 5 na baadae tufanye vizuri michuano ya ubingwa wa Afrika ili tuwe na msingi mzuri wa kushindana kutafuta nafasi ya kushiriki Olimpiki 2016.
Mhe. Rais Kikwete aliishauri TBF iendeleze mahusiano mazuri na wafadhili walioko ikiwamo kampuni za Coca Cola, TBL na wengine na pia pale atakapopata nafasi atajitahidi kuongea na wakuu wa makampuni hayo namengine ili waongeze ufadhili wao kwa TBF.

Mhe Rais Kikwete aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuendeleza mchezo wa kikapu na akaomba tusisite kumtumia pale tutakapohitaji msaada wake au wa Serikali.

TBF inamshukuru sana Rais Kikwete kwa mwaliko huu na utayari wake wa kushirikana na vyama vyote michezo katika kuendeleza michezo na husuani mchezo wa huu wa kikapu, na TBF inaomba wadau wote wa michezo na maendeleo waunge mkono jitihada hizi kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version