Klabu ya Manchester United inajivunia kuwa ndio klabu ya soka yenye mataji mengi Zaidi miongoni mwa vilabu ambavyo vilivyoko nchini Englanda. Katika mataji ambayo iliyowahi kuyapata mengi ya mataji hayo waliyapata wakati kikosi hicho kikiwa chini ya kocha mkuu Sir Alex Ferguson. Kocha huyo ndiye kocha ambaye anayeongoza kwa kubeba mataji mengi duniani. Chini ya kocha huyo waliingia mara 4 kwenye fainali za klabu bingwa ulaya na wakabeba mara 2 na kisha kushindwa kubeba mara 2.
Katika hizo mara 2 ambazo walishindwa kubeba walishindwa dhidi ya klabu ya Barcelona ya mwaka 2009 na walibeba mwaka 1999 na kisha kubeba tena mnamo mwaka 2008 walipoifunga klabu ya Chelsea kwenye fainali ambayo ilikuwa ina msisimko mkubwa sana. Katika kijitabu cha tawasifu (AUTOBIOGRAPHY)) ya maisha yake huwa anajivunia sana mafanikio yake kwenye soka kwa kuzungumzia maamuzi magumu ambayo alianza nayo kazi mnamo mwaka 1986 baada ya kukabidhiwa klabu hiyo na aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo bwana Martin Edwards. Mojawapo ya maamuzi magumu ambayo aliyafanya ni kuanza kubana matumizi kwa klabu hiyo na kuachana na sera ya kuanza kusajili wachezaji wenye majina makubwa na kasha kuanza kutumia maskauti wapya ambao aliwapa kazi ya kutafuta wachezaji chipukizi ambao wangekuja kuleta mageuzi katika klabu hiyo kwa siku za usoni.
Maskauti hao walianza kuzunguka katika miji mbalimbali nchini England na maeneo jirani na kasha kuwaletea wachezaji mbalimbali ambao hao walikuja kusajiliwa na klabu hiyo. Wachezaji ambao waliletwa katika nyakati hizo ni pamoja na David Beckham, Nick Butt, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville na Paul Scholes.wachezaji hawa kwa pamoja kizazi chao kilikuja kupewa jina la Class of 92. Waliitwa hivyo kwa minajili ya kukumbuka mwaka ambao walianza kuchezea klabu hiyo. Wachezaji hao walisaidia sana klabu hiyo kupata mafanikio na program hiyo ilizaa matunda sana mnamo mwaka 1999 kwani klabu ya Manchester United ilifanikiwa kutwaa mataji 3 tofauti ndani ya msimu mmoja.
Klabu ya Azam FC ambayo yenye maskani yake katika kitongoji cha Chamanzi jijini Dar es salaam wakati inaanza kucheza ligi kuu ilikuwa ina program kabambe ya kuwapa nafasi wachezaji wadogo ambao walikuwa wamekuzwa kisoka katika kituo chao cha kulea wachezaji(academy) ambacho kilikusanya wachezaji ambao walitolewa maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania. Klabu hiyo ilikuwa inasifika kwa kuzalisha wachezaji kama vile John Bocco(adebayor), Himid Mao mkami, Salum Abubakar(Sure boy), Aishi Manula, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Novatus Dismas, Simon Msuva, Mudathir Yahya na wengineo. Akademi ya Azam ilisifika afrika mashariki nzim kwa kuzalisha wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kwa miaka kadhaa. Uongozi wa klabu hiyo uliwekeza vizuri kwenye akademi hiyo kwa kuanza kuweka miundombinu mizuri na pia hata uwekezaji katika rasilimali watu kwani makoca na walezi wa kituo hicho walikuwa ni watu wenye vigezo vikubwa. Waliweka mfumo mzuri wa maskauti ambao waliwaletea wchezaji ambao wenye vipaji na pia walikuwa wana umri mdogo.
Uwekezaji huo uliwasaidia kwenye msimu wa mwaka 2013/2014 klabu ya Azam iliweza kuibuka kuwa ndio mabinwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni miaka 6 toka kuanzishwa kwake na kikosi chao cha kwanza kilikuwa kina wachezaji kadhaa ambao walikuwa wamekulia toka kwenye akademi yao pamoja na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wamewasajili toka maeneo mbalimbali ambao walikiongezea nguvu kikosi chao.
Ubingwa huo waliupata mnamo mwezi Aprili baada ya kuirfunga klabu ya Mbeya City na hatimaye kuwa wanaongoza ligi kwa idadi ya pointi ambazo hakuna klabu nyingine ambayo ingeweza kuzifikia pointi hizo. Mnamo Aprili 4 ya mwaka 2013 klabu hiyo ilijivunia kupitia kurasa zake za jamii kwamba katika kikosi ambacho kilitangazwa cha timu ya taifa ya vijana ya nyakati hiyo wachezaji 11 ambao walijiunga na kambi ya timu ya taifa walipitia katika akademi ya klabu hiyo. Wachezaji hao ilikuwa ni pamoja na Aishi Manula, Hamed Juma, ismail Adam Gambo, Mohammed Shabalala, Mgaya Abdul, Mudathiri Yahya, Farid Musa, Joseph Kimwaga, Dismas Yushi na Reyna Mgunsila.
Baada ya mda si mrefu toka wapate mafanikio ya kuwa bingwa wa ligi kuu soka bara klabu hiyo iliuza wachezaji wake muhimu katika vilabu kadhaa na huku wengi wao wakiuzwa kwenye klabu ya Simba ambapo ilipelekea baadhi ya wadau kujenga hoja ya kwamba klabu hiyo ilipeleka wachezaji wake muhimu kwa klabu ya Simba ili kuisaidia klabu hiyo katika mashindano ya kimataifa.
Waliwauzia klabu ya Simba wachezaji wafuatao: John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe, erasto Nyoni, Pascal Wawa n.k ambao wachezaji hawa waliisaidia klabu ya Simba kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania mara nne mfululizo na hatimaye kufika hadi hatua ya makundi katika klabu bingwa ya soka barani Afrika. Simba imepata mafanikio makubwa kwa kuwatumia classs of 92 ya Azam lakini Azam haijaweza kupata mafanikio makubwa sana Zaidi ya sifa tu kwamba wachezaji hao walipitia katika akademi yao na mpaka sasa hawana hata mchezaji mmoja ambaye yuko kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ambaye wanayaweza kujisifia kwamba amepitia katika mfumo wa akademi wa klabu hiyo.