Menu
in

Chezea Simba wewe….!

Magoli kutoka kwa mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’  yaliwapa Simba mwanzo mzuri dhidi ya ES Setif ya Algeria katika mechi yao ya awali ya hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Mbele ya mashabiki 41,053 wa nyumbani, Simba ilisubiri hadi dakika 18 za mwisho kupata uongozi wa magoli mawili ya kwenda nao mjini Algiers Aprili 6 kwa ajili ya mechi yao ya marudiano.

Okwi aliwafungia wenyeji goli la kuongoza katika dakika ya 72 akimalizia pasi fupi ya Boban aliyekuwa amebanwa na mabeki wa Setif na dakika saba baadaye Simba walikuwa mbele kwa magoli 2-0 kupitia kwa Boban alifunga kufuatia pasi ya Felix Sunzu aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Mohammed Benhamou.

Simba walitawala sehemu kubwa ya mchezo hasa kipindi cha pili wakati Setif, ambao walielezea hofu ya kusumbuliwa na hali ya hewa ya joto kwa kuwa kwao kuna baridi wakati huu walionekana kuchoka tangu kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, walikuwa ni Setif walioanza vizuri mechi na katika dakika ya kwanza tu, beki wa kati wa Simba, Juma Nyosso alifanya kazi nzuri kwa kutoa nje mpira ulipigwa na kiungo wa Setif, Mourad Dechmoussa, ambaye alimtoka beki wa pembeni, Amir Maftah.

Kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda, Simba ndivyo walivyozidi kutawala mchezo.

Okwi alishindwa kuipatia Simba goli la mapema katika dakika ya 4 wakati kichwa chache kiliposhindwa kulenga lango kufuatia krosi ya Salum Machaku na katika dakika 12 kipa wa Setif, Benhamou, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Algeria alidaka shuti la Sunzu na kuinyima Simba goli.

Chelewa ufike, wahenga walisema, na Simba ilisubiri hadi dakika za lala salama kupata ushindi iliouhitaji.

Kabla ya kuanza kwa mechi, NIPASHE ilishuhudia watu waliotuhumiwa kuuza tiketi ‘feki’ wakiwa wamekamatwa na kupandishwa katika karandinga la polisi.

Vikosi vilikuwa: Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Patrick Mafisango/ Jonas Mkude (dk. 89), Salum Machaku, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu/Gervais Kago (dk. 89), Haruna Moshi ‘Boban’ na Emmanuel Okwi.

Setif: Mohammed Benhamou, Riadh Benchad, Smain Diss, Farouk Beckaid, Mourad Dechoum, Mokhtar Benmoussa, Racid Ferrali, Youcef Ghezzali, Youssef Sofiane/ Mohammed Tiouli (dk.57), Mokhtar Megueni na Abderrahmane Hachoud.

Na Somoe Ng`itu
26th March 2012
B-pepe
Chapa
Maoni
Machaku Salum wa SImba (Kulia) akikwaana na mchezaji wa ES Setif ya Algeria wakati wa mechi yao ya awali ya hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam jana. Simba ilishinda 2-0.

Magoli kutoka kwa mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’  yaliwapa Simba mwanzo mzuri dhidi ya ES Setif ya Algeria katika mechi yao ya awali ya hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Mbele ya mashabiki 41,053 wa nyumbani, Simba ilisubiri hadi dakika 18 za mwisho kupata uongozi wa magoli mawili ya kwenda nao mjini Algiers Aprili 6 kwa ajili ya mechi yao ya marudiano.

Okwi aliwafungia wenyeji goli la kuongoza katika dakika ya 72 akimalizia pasi fupi ya Boban aliyekuwa amebanwa na mabeki wa Setif na dakika saba baadaye Simba walikuwa mbele kwa magoli 2-0 kupitia kwa Boban alifunga kufuatia pasi ya Felix Sunzu aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Mohammed Benhamou.

Simba walitawala sehemu kubwa ya mchezo hasa kipindi cha pili wakati Setif, ambao walielezea hofu ya kusumbuliwa na hali ya hewa ya joto kwa kuwa kwao kuna baridi wakati huu walionekana kuchoka tangu kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, walikuwa ni Setif walioanza vizuri mechi na katika dakika ya kwanza tu, beki wa kati wa Simba, Juma Nyosso alifanya kazi nzuri kwa kutoa nje mpira ulipigwa na kiungo wa Setif, Mourad Dechmoussa, ambaye alimtoka beki wa pembeni, Amir Maftah.

Kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda, Simba ndivyo walivyozidi kutawala mchezo.

Okwi alishindwa kuipatia Simba goli la mapema katika dakika ya 4 wakati kichwa chache kiliposhindwa kulenga lango kufuatia krosi ya Salum Machaku na katika dakika 12 kipa wa Setif, Benhamou, ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Algeria alidaka shuti la Sunzu na kuinyima Simba goli.

Chelewa ufike, wahenga walisema, na Simba ilisubiri hadi dakika za lala salama kupata ushindi iliouhitaji.

Kabla ya kuanza kwa mechi, NIPASHE ilishuhudia watu waliotuhumiwa kuuza tiketi ‘feki’ wakiwa wamekamatwa na kupandishwa katika karandinga la polisi.

Vikosi vilikuwa: Simba: Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Patrick Mafisango/ Jonas Mkude (dk. 89), Salum Machaku, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu/Gervais Kago (dk. 89), Haruna Moshi ‘Boban’ na Emmanuel Okwi.

Setif: Mohammed Benhamou, Riadh Benchad, Smain Diss, Farouk Beckaid, Mourad Dechoum, Mokhtar Benmoussa, Racid Ferrali, Youcef Ghezzali, Youssef Sofiane/ Mohammed Tiouli (dk.57), Mokhtar Megueni na Abderrahmane Hachoud.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version