Menu
in , ,

Chelsea wawapandia Man U

Pedro

*Van Gaal mguu mmoja UCL

Wakati Manchester United wameshinda mechi ya mkondo wa kwanza kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), wametikiswa na Chelsea wamewapandia dau kumtwaa mshambuliaji wa Barcelona, Pedro, aliyekuwa njiani kwenda Old Trafford.

Man U walishinda 3-1 kwenye mechi iliyofanyika nyumbani kwao dhidi ya Club Brugge, mabao mawili yakifungwa na mchezaji wao mpya, Memphis Depay, moja likiwekwa kimiani na Marouane Fellaini wakati pia wakijifunga wenyewe kupitia kwa Michael Carrick.

Brugge waliwatisha United, kwani ndio walioanza kupata bao mapema dakika ya nane, na walionekana kudhamiria kuwatuliza Man U lakini jitihada za wenyeji zilizaa matunda, huku mchezaji wa Brugge, Brandon Mechele, akitolewa nje kwa kadi nyekundu karibu na mwisho wa kipindi cha pili.
sw

Wakati United wakifurahia hayo na kusubiri mechi ya mkondo wa pili ugenini ambayo yaelekea itakuwa kali, Chelsea wameingilia mipango yao iliyokuwa ikienda vyema ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Barcelona, Pedro na habari zinasema kwamba wamewapokonya Man U mchezaji huyo.

Habari zinasema kwamba matajiri hao wa londo watamsajili winga huyo kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 21. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa na kila dalili ya kwenda Old Trafford, lakini sasa yaelekea gia imebadilishiwa angani na anaelekea London kukamilisha mipango ya usajili.

Pedro alianzia kwenye akademia ya Barca, ambapo hadi sasa amefunga mabao 99 katika mechi 326 tangu alipojiunga nao 2008. Aliwaambia klabu anataka kuondoka kwa ajili ya kupata muda zaidi wa kucheza, kwani Camp Nou alikuwa akizingwa na akina Neymar, Lionel Messi na Luis Suarez hivyo kukosa namba.

Chelsea pia wanataka kumsajili mlinzi wa kati wa England na Everton, John Stones, japokuwa wamekataliwa mara tatu ofa zao, kuanzia pauni milioni 20, kisha milioni 26 na jana tu pauni milioni 30, Everton wakisisitiza hauzwi.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version