Menu
in , , , ,

Chelsea wapita kiaina Ulaya

*Real waponea chupuchupu

Chelsea wamefanikiwa kufika nusu fanali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (UCL) baada ya kuwatoa Paris Saint-Germain.
Katika mazingira ambay hayakutarajiwa, Chelsea walibadilisha mwelekeo wa mchezo ambapo kwenye mechi ya kwanza nchini Ufaransa walifungwa 3-1.

Katika mechi ya usiku wa Jumanne iliyofanyika Stamford Bridge jijini London. Chelsea walishinda kwa mabao 2-0 na kufanya uwiano wa mabao kuwa 3-3 na Chelsea kufaidika kwa bao la ugenini.

Alikuwa ni mshambuliaji asiyeaminika mbele ya Kocha Jose Mourinho, Demba Ba aliyewavusha Chelsea dakika tatu tu kabla ya mchezo kumalizika kw abao lake safi.

Kiungo Andre Schurrle ambaye ‘The Happy One’ alipata kusema ni bora kuliko washambuliaji wake alifanya kazi aliopangiwa kwa kufunga bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza.

Mipira ya Mjerumani huyo na Mbrazili Oscar iligonga mwamba wa goli katika jitihada za kuwapatia Chelsea mabao na ikawa imeonekana kwamba Chelsea wangemaliza mechi wakiwa nyuma.

Katika mechi nyingine, Real Madrid wamefanikiwa kuvuka kuingia nusu fainali baada ya kupambana dhidi ya Borussia Dortmud.
Madrid ambao walishinda 3-0 kwenye mechi ya kwanza hawakuona tabu kupoteza kwa 2-0 usiku wa Jumanne, kwani walisonga mbele kwa tofauti ya bao hilo moja.

Madrid wangeweza kuwaduwaza Wajerumani hao mapema, lakini penati ya Angel Di Maria iliota mbawa na kuwafanya wageni hao kuwa na kazi ngumu wakipaya huduma ya kipa Iker Casillas.

Hata hivyo, licha ya mabao ya Marco Reus katika dakika ya 24 na 37 yaliwasababishia kihoro vijana wa Carlo Ancelotti lakini hatimaye wakavuka kw atofauti ya pointi moja.

Katika mechi nyingine za marudiano ya robo fainali, Bayern Munich wanavaana na Manchester United wakati Atletico Madrid wakiwakaribisha Barcelona.
Bayern walitoka sare ya 1-1 na Man U kwenye mechi ya kwanza wakati Atletico nao waliwalazimisha Barca sare kama hiyo kwenye mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Camp Nou.

51.577972-0.130407

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version