MATUMAINI ya Afrika kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia yameendelea kufifia baada ya Cameroon kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Japan katika mchezo wa Kundi E uliochezwa jana mjini Bloemfontein.
Bao la kipindi cha kwanza la Keisuke Honda lilitosha kuinyima raha Cameroon ambayo katika mchezo wa jana ilichezesha damu mpya kadhaa ambazo zimeonyesha hata hivyo kubadili mchezo wa timu hiyo.
Kwa muda mrefu, wawakilishi hao wa Afrika ambao wameungana na Nigeria na Algeria kuanza kwa kipigo katika michuano hiyo walihangaika kupita ukuta mgumu wa Japan ambayo imeweka rekodi ya kupata ushindi wa kwanza wa fainali za Kombe la Dunia nje ya eneo lake.
Katika mchezo wa mapema mchana, Uholanzi iliilaza Denmar kwa mabao 2-0 huku beki MtanzaniaPatrick Mtiliga wa Denmark akiwa mtazamaji mbele ya mashabiki 83,465 waliojitokeza kwenye Uwanja wa Soccer City jijini.
Katika mchezo huo, Uholanzi ilitawalasehemu kubwa ya mchezo, timu hiyo ilisubiri kipindi cha pili kupata mabao yake.
Mtiliga ambaye baba yake ni Mtanzania anaichezea Denrmark ambayo ni nchi ya mamayake, lakini katika mchezo huo akiwa amevaajezi namba 23 alijikuta akiishia benchi.
Hata hivyo katika mchezo huo wa Kundi E,timu hizo zilianza mchezo kwa kupooza na wachezaji kuzubaa, lakini Denmark licha ya kuzidiwa,ilionekana kufanya mashambuzi ya hatari zaidi kipindi cha kwanza kupitia kwa Nicklas Bendtner na Dennis Rommedahl.
Mchezo ulibadilika kipindi cha pili na Uholanzi walionekana kuja kwa kasi na dakika moja tangu kuanza kwa kipindi hicho, Robin VanPersie alipiga krosi kutoka upande wa kushoto ambayo ilimkuta beki wa SimonPoulsen wa Denmark aliyejifunga kwa kichwa katikaharakati za kuokoa.
Beki huyo alipiga kichwa fyongo na mpira ukaenda kumbabatiza beki mwenzake, Daniel Agger nakumchanganya kipa wao,Thomas Sorensen.
Bao la pili la Uholanzi lilifungwa kirahisi na Dirk Kuyt dakika ya 85 baada ya kumalizia mpira uliogonga mwamba na kurudi uwanjanikutokana na kazi nzuri ya Eljero Elia aliyeichambua ngome ya Denmark kabla ya kupiga shuti kali lililogonga mwamba.
Uholanzi ilifanya mashambulizi mengi katikamchezo huo kupitia washambuliaji wake nyota;Van Persie, Wesley Sneijder na Rafael Van Der Vaart.
Sneidjer ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo angefunga bao dakika ya 81, lakini shuti lake liligonga mlingoti ya juu na kuwa kona isiyo na matunda.
Kwa mujibu wa taarifa ya Fifa kwa waandishi wa habari, Uholanzi ilimiliki mchezo huo kwaasilimia 58 huku Denmark ikipata asilimia 42.