Moja ya wawakilishi wa Afrika kwenye Kombe la Dunia, Cameroon, wamefanya vyema kwenye mechi za kirafiki zilizofanyika.
Licha ya nahodha wao, Samuel Eto’o kupumzishwa kutokana na matatizo ya majeraha, Simba Wasiofugika walifanya vyema kwenye mechi yao dhidi ya Macedonia iliyochezwa Austria.
Haikuwa siku nzuri kwa Cameron, kwa sababu mpachika mabao wao mwingine, Pierre Webo (32) aliumia bega baada ya kuwafungia Cameroon bao la kwanza.
Jean-Eric Maxim Choupo-Moting, bila kujali urefu wa jina lake, ndiye alifunga bao la pili kwa Cameroon kutokana na ulinzi dhaifu wa Macedonia.
Cameroon walilazimika kuwaacha nje ya uwanja kipa Charles Itandje, mlinzi Jean-Armel Kana-Biyik na viungo Edgar Salli, Jean II Makoun na Stephane Mbia kutokana na maumivu, japo madogo.
Mechi hiyo ilichezwa licha ya kutokuwapo makubaliano baina ya wachezaji na Shirikisho la soka la Cameroon.
Wanaanza kibarua kwenye Kombe la Dunia kwa kukipiga na Mexico Juni 13katika mji wa Natal, Brazil, lakini wana mechi nyingine za kujiandaa dhidi ya Paraguay, Germany na Moldova.
Katika mechi nyingine za kirafiki, Australia walikwenda sare ya 1-1 na Afrika Kusini, Urusi wakawafunga Slovakia 1-0 na Montenegro na Iran wakatoka suluhu.
Matokeo mengine ni kwa Estonia na Gibraltar kwenda sare ya 1-1 Ubelgiji walikuwa wacheze na Luxembourg na Serbia na Jamaica.