in ,

Buriani Bobbi Kristina

Bobbi Kristina amefariki dunia. Huyu ni binti wa mwanamuziki hayati Whitney Houston aliyefariki katika mazingira yale yale ya bintiye.

Mwakilishi wa familia, Kristen Foster amesema kwamba Christina, 22, aliaga dunia akiwa amezungukwa na familia yake na kwamba “hatimaye yupo kwa amani katika mikono ya Mungu.”

Msichana huyu alikutwa akiwa hajitambui Januari 31 mwaka huu bafuni na tangu wakati huo hajapata kuzinduka lakini alikuwa hai hadi Jumapili hii, akafia Duluth, Georgia alikohamishiwa huko kwa ajili ya huduma maalumu lakini afya yake ilizidi kuzorota.

Kristina ndiye binti pekee kwa Houston na mwimbaji wa muziki wa miondoko ya R&B, Bobby Brown. Houston alikutwa amekufa katika bafu la hoteli jijini Los Angeles 2012 na inasadikiwa kwamba alikuwa amekunywa kilevi kupita kiasi. Bintiye anadhaniwa kuwa kwenye mazingira hay ohayo.

Truly sad gone too soon I hope shes at peace with her mom
Truly sad gone too soon I hope shes at peace with her mom

“Ni vigumu kusema kwa heri. Jumapili ya Julai 26, Bobbi Kristina aliondoka katika dunia hii kwa amani. Familia inamshukuru kila mmoja kwa upendo na sala. Kama ambavyo Bobbi Kristina angesema: ‘Upepo umeshanipita bali Jua lipo usoni mwangu’.

Wanamuziki na watu maarufu walianza kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia, wengi waksiema kwamba watakosa muda mzuri wa kuwa naye. Alisema 2012 kwamba alitaka kuiga na kufanya kwa ufanisi kazi ya mama yake ya kuimba na kucheza lakini hakufanikiwa kutekeleza ndoto hiyo.

Alianza sanaa na mama yake 1999, akiimba ‘My Love is Your Love’ na ‘Little Drummer Boy’. Tangu kufariki dunia kwa mama yake, Kristina alipelekwa hospitali mara mbili kwa kuonesha dalili za kujawa wasiwasi na kuchanganyikiwa.

Kristina alikuwa akiishi Atlanta na Nick Gordon, mwanamume aliyemtambulisha kuwa mume wake. Polisi walielezea tatizo lililomfika bafuni kuwa ni kuzama kwenye maji. Wakati huo hakudhaniwa kwamba alikuwa anapumua ambapo alikuwa kaelekeza kichwa chini kwenye bafu hilo na alikuwa na mikwaruzo mwilini mwake.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi polisi walijiridhisha kwamba hakuwa ameumizwa, bali mikwaruzo usoni na mdomoni ilitokana na ajali ya gari siku kadhaa kabla ya kupatwa tatizo hilo.

Uchunguzi wa kitabibu utafanyiwa mwili wake ili kutambua kilichosababisha kifo chake, lakini wataalamu wa uchunguzi aina hiyo wanasema muda uliopita tangu alipopoteza fahamu hadi kifo chake utasababisha shida katika kubaini sababu halisi ya kifo hicho.

Uhusiano wa Kristina na Gordon uliingia matatizo kutokana na madai ya Kristina kwamba alikuwa akimhujumu. Anadaiwa kugamisha dola 11,000 kutoka kwenye akaunti ya binti huyo kwenda kwenye akaunti inayodhibitiwa na Gordon mwenyewe wakati Kristina akiwa hospitalini.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

ROBO FAINALI KAGAME KUANZA KESHO

MOBUTU ALIVYOPELEKA MATUMAINI ANFIELD