Menu
in , , ,

Brazil wajaribu kufuta machozi

Brazil wanawavaa Uholanzi kutafuta mshindi wa tatu katika fainali za Kombe la Dunia, wakiwa na dhamira ya kuwafuta machozi washabiki wake baada ya kichapo cha 7-1 kutoka kwa Ujerumani kwenye nusu fainali.

Kocha Luiz Felipe Scolari amesema kwamba wamejipanga vyema kwa mechi hiyo, kutakuwa na mabadiliko kadhaa na wala hawaichukulii kwa mzaha au udogo wa hadhi kwa namna yoyote ile.

Brazil wanakutana na Uholanzi wanaofundishwa na Louis van Gaal ambaye amesema wazi kwamba haoni mantiki ya mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, kwani hadhi pekee ya ushindi ni kwua bingwa na si vinginevyo.

Uholanzi walitolewa kwa penati na Argentina katika nusu fainali ambapo Wadachi walifanikiwa kupiga shuti moja tu langoni mwa Argentina.

Nahodha wa Brazil, Thiago Silva ataongoza ukuta wa taifa hilo, baada ya kuikosa mechi waliyopokea kipondo kutoka Ujerumani kwa sababu ya kuwa na kadi mbili za njano.

 Brazil walijaribu kuikatia rufaa kadi ya pili ikashindikana, ambapo pia Brazil walimkosa nyota wao wa kipekee, Neymar aliyetenguliwa mgongo wakati wa mechi baina yao na Colombia kwenye robo fainali.

Van Gaal anayeanza kazi mpya kuwanoa Manchester United anaweza pia kubadili wachezaji wake, hivyo si ajabu akina Memphis Depay na Klaas-Jan Huntelaar wakaanza badala ya wale wa kawaida kama Robin van Persie.

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ilianzishwa mara ya kwanza 1934, na awali ilikuwa kama mechi tangulizi ya ile ya fainali, kuwaweka watu sawa, na Van Gaal anasema kitu kibaya zaidi katika mechi kama hiyo ni kwamba timu moja inaweza lazima ipoteze mfululizo, yaani baada ya kufungwa kwenye nusu fainali.

Uholanzi waliana vyema michuano hii kwa kuwafunga mabingwa watetezi waliotema kombe, Hispania mabao 5-1 lakini baada ya hapo walibanwa licha ya kufuzu. Brazil walianza kimkanda mkanda hadi wakatolewa kwa aibu, ukiachilia mbali ushindi mkubwa dhidi ya Cameroon.

Hii itakuwa mechi ya 12 baina ya Brazil na Uholanzi, ya tano katika fainali za Kombe la Dunia. Wadachi walishinda mechi mbili kati ya tatu za karibuni za Kombe la Dunia, ikiwa ni pamoja na 2-1 katika robo fainali ya 2010.

Mataifa haya mawili ndiyo yamecheza rafu nyingi zaidi katika mashindano, Brazil wakizifanya mara 107 na Uholanzi mara 106.

Ushindi wa mwisho wa Brazil dhidi ya Uholanzi ni 1999 kwa mabao 3-1. Kwenye mechi hiyo, wachezai watano walipewa kadi nyekundu, ambao ni Edgar Davids, Andre Ooijer na Peter van Vossen wa Kidachi na pia Rivaldo naAmoroso wa Brazil.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version