Menu
in , , ,

Brazil: Tupo tayari

Brazil ipo tayari kwa kishindo cha Kombe la Dunia linaloanza Alhamisi hii.

Baada ya pilika za maandalizi ya kujenga viwanja, kuboresha miundombinu, kupoza wanaogoma na kupokea wageni, sasa muda umewadia kwa kazi kuanza.

Rais Dilma Rousseff ameiambia dunia kwamba kila kitu kipo tayari na waliokuwa wanaitakia nchi mabaya wameshindwa na kwamba hakuna utata wowote.

Anasema kwamba watu wa Brazil wana dhamira kubwa ya kuwa wenyeji wema na bora wa mashindano haya makubwa zaidi duniani na kwamba yataacha urithi usioisha katika miundombinu na ukuaji uchumi.
Pamekuwa na migomo, ikiwamo ya wafanyakazi wa treni hivyo kuhatarisha usafiri katika mechi ya ufunguzi Sao Paulo na fainali Rio de Janeiro.

Mkuu wa Kamati ya Kombe la Dunia ya Brazil, Ricardo Trade amesema kwamba mamlaka zipo tayari kuhakikisha kila kitu kinakwenda kilivyopangwa ndani na nje ya uwanja.
Rais Rousseff aliwashangaa watu wanaodai kwamba Brazil imeingia hasara kwa kuandaa mashindano hayo, akisema wageni hawataondoka na miundombinu kwenye mabegi yao na pia uchumi utakua kwa kiasi kikubwa kutokana na mashindano hayo.

Uingereza ilipoandaa michuano ya Olimpiki miaka miwili iliyopita, ilitumia fedha nyingi lakini baadaye wananchi wameanza kufaidika kwa miundombinu kuboreshwa lakini pia kwa uchumi kukua kwa kiasi kikubwa.

Brazil imetumia dola bilioni 11 kuandaa mashindano hayo lakini inatarajia kwamba italipa kwa njia mbalimbali na pia imeenzi utamaduni wa taifa hilo ambalo ni maarufu kwa soka tangu enzi na enzi.

“Katika jezi za kijani na njano tunawakilisha urithi mkubwa na wa ajabu wa watu wa Brazil,” akasema rais huyo na kuongeza kwamba bajeti ya kati ya mwaka 2010 na 2013 katika maeneo mengine ilikuwa kubwa kuliko uwekezaji uliofanywa katika viwanja na miundombinu.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version