Menu
in , , ,

Brazil robo fainali

 

*Julio Cesar aibuka shujaa

*Colombia wawafyatua Uruguay

 

Cezar aliwaokoa maelfu ya Wabrazil waliokuwa roho juu uwanjani na majumbani baada ya Samba Boys kubanwa mbavu na Chile katika dakika 120 za awali.

 

Waliingia katika changamoto ya mikwaju ya penati kutokana na kwenda sare ya 1-1 katika muda wa kawaida na kushindwa kufungana kwenye dakika 30 za ziada.

 

George Sampaoli wa Chile aliwaanzisha wachezaji wake wakicheza taratibu na kuwaacha Brazil waendelee na shinikizo lao.

 

Hata hivyo, David Luiz aliwainua vitini Wabrazili na washabiki wao wengine kwa kutikisa nyavu kutokana na kona ya Neymar lakini Alex Sanches alisawazisha baada ya mabeki Luis Gustavo, Marcelo na wengineo kuzidiwa maarifa na Chile waliogongeana pasi tatu eneo la robo ya Brazil.

 

Kwa ufundi na mbinu ni kwamba timu zote mbili zilionekana kuwa na nguvu sawa licha ya kucheza tofauti na kila mchezaji akijitahidi kutetea taifa lake.

 

Kwa mizania ya ufundi, Brazil walijitahidi kushambulia lakini wakakosa umakini katika kulinda lango.

 

Hata hivyo dakika za mwisho mwisho Chile walionekana kuchoka na wakawa kana kwamba wanaanguka.

 

Kipa Claudio Bravo wa Chile ambaye ndiye nahodha, alikuwa mahiri na kuokoa mabao ya wazi ya wachezaji wa Brazil, akiwamo Neymar.

 

Brazil wangeweza kutoka kifua mbele ndani ya dakika 90 kama si mwamuzi Howard Webb kubadili uamuzi na kukataa bao la Hulk wa Brazil baada ya kushawishiwa na mwamuzi msaidizi na Mwingereza mwenzake Michael Mullarkey aliyedai kwamba kabla Hulk hajacheka na nyavu aliunawa mpira japokuwa ilioekana kama vile aliweka gambani na si mkononi.

 

jamaa hao wa Amerika Kusini walipoingia hatua ya kupigiana penati, Brazil walitoka mbele kwa 3-2. Wafungaji wa Brazil walikuwa David Luiz, Marcelo na Neymar.

 

Willian anayechezea Chelsea alitoa nje mkwaju wake licha ya kumpeleka kipa ‘marikiti’ na penati ya Hulk iliokolewa na kipa Bravo.

 

Colombia wawafyatua Uruguay

20140629-132242-48162631.jpg

 

Colombia wamefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuwalaza Uruguaya 2-0.

 

Wakicheza bila shujaa wao, Luis Suarez aliyefungiwa kwa utovu uliokithiri wa binadamu, Uruguay waliwatumia mkongwe Diego Forlan na Edinson Cavani lakini pengo lilionekana dhahiri.

 

Chipukizi James Rodriguez alidhihirisha kwamba anapanda chati kimataifa, kwa kufunga mabao mawili.

 

Bao la kwanza lilikuwa lenye mvuto wa aina yake kutokana na ufundi aliotumia akichanganya na kipaji chake na kumweka juu akiwaelekea akina Lionel Messi na Neymar.

 

Colombia watakabiliana na wenyeji Brazil kwenye mechi ya robo fainali, ambapo katika mechi ya awali Brazil waliwafunga Chile kwa penati 3-2 baada ya kwenda sare ya 1-1 katika dakka 90 za kawaida na 30 za ziada.

 

Timu zote zilizocheza Jumamosi hii zinatoka Amerika Kusini, ambapo inaonekana kwamba zimedhamiria kubakisha kombe nyumbani, lakini mwelekeo zaidi utapatikana baada ya mechi zote za 16 bora kumalizika.

Cezar alidaka penati mbili za kwanza, akaruhusu mbili nyingine kutinga wavuni huku akiifuata ya mwisho ambayo ilikwenda mbali naye na kuishia kugonga mwamba na kutoka nje.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version