Menu
in

Bingwa Kikapu Apatikana Bongo

Bingwa wa kikapu

Kumekuwa na jitihada za makusudi kwa viongozi wa mchezo wa mpira wa kikapu Tanzania kuendeleza mchezo huo ili upate thamani inayohitajika.

Viongozi wao akiongozwa na Rais Pharesi Magesa pamoja na kocha Bahati Mgunda wamekuwa mstari wa mbele kupigania mchezo huu ili ufike pale wanapohitaji.

Licha ya changamoto nyingine za kibinadamu katika mgawanyo wa majukumu kulingana na katiba ya chama hicho bado wanafanya vizuri kwa kadri wanavyoweza.

Hivi karibuni wameimaliza ligi ya mchezo huo na kila aliyeshiriki amepongeza jitihada za dhati kwa uongozi.

Wengi walikuwa wanasubiri timu gani itaibuka bingwa ili ziwakilishe taifa katika michuano ya klabu bingwa ya mchezo huo.

Hii ifutayo ni majumuisho tokeo ya hitimisho la mchezo huo kabla ya kuanza na michuano mingine ambapo ratiba utaona hapo chini katika maelezo ya matokeo.

Timu ya Kurasini Heats imetwaa taji la ubingwa wa kikapu Tanzania (National Basketball League – NBL 2020) kwa kuifunga Oilers 76-59.

Wakati huo  nafasi ya mshindi wa tatu imeenda kwa Don Bosco Panthers ya Dodoma kwa kuifunga Vijana Basketball Club ya Dar es Salaam 80-77.

Kwa upande wa Wanawake JKT imetwaa Ubingwa huo na mshindi wa pili ni Don Bosco Lioness zote za Dar es Salaam.

Bingwa wa NBL Wanaume atawakilisha Tanzania katika mashindano ya kombe la klabu bingwa ya Afrika (Basketball Africa League – BAL) na mshindi wa pili na wa tatu watawakilisha katika mashindano ya vilabu ya kanda ya tano ya Afrika (Zone V Club Championship /Challenge Cup).

Kwa  upande wa wanawake bingwa na mshindi wa pili wote watawakilisha katika mashindano ya vilabu ya wanawake ya kanda ya tano ya Afrika.

Msimu wa ligi ya Vilabu ya Kikapu ya Tanzania ( NBL) ilianza mwezi Februari mwaka huu kwa ngazi za mikoa (RBA) na imemalizika rasmi 25 Oktoba, 2020 kwa ngazi ya Taifa.

“Sasa tunaendelea maandalizi ya Taifa CUP 2020, mashindano ya kombe la Taifa yanakayoshirikisha timu za mikoa yanayotarajiwa kufanyika 12-21 Novemba, 2020 Dodoma,”.

Kauli mbiu yao juu ya mchezo huu ni kwamba ‘Kikapu ni zaidi ya game ni maisha’.

Mchezo huu unaweza ukawa na faida kubwa kwa taifa endapo ukiangaliwa kwa makini, kama timu za mpira zinashindwa kupata nafasi ya kushiriki huko kimataifa wakati zikiwa na udhamini mnono, huku katika kikapu nako sehemu sahihi sana kuwekeza.

Bahati Mgunda amewahi kusema kuwa huku pia kuna fursa mbalimbali za vijana kupata nafasi hata ya kushiriki kimataifa kutokana na njia yyake ya kuingia sio ngumu sana kama ilivyo michezo mingine.

Aliwahi kuweka wazi kuwa ukosefu wa udhamini ndio sababu kubwa ya kutofanya vizuri, lakini pia ametoa rai kwa wanahabari kutoa habari za mchezo huu mara kwa mara ili uweze kuwaingia akilini na hatimaye kuupenda.

Katika mchezo huu bado hatujapata wakumzidi Hasheem Thabeet katika  hivyo vijana watumie fursa mbalimbali zinazojitokeza ili wapate nafasi za kuonekana kama ilivyokuwa kwa Hasheem.

Uhai wa mchezo huu sio kuwaachia viongozi bali kuungana kwa pamoja kuusogeza mbele kwa kuutangaza pamoja na kuufanya uwe pendwa kama inavyofanyika katika michezo mingine.

Hadi sasa nguvu kubwa imewekwa na viongozi wa mchezo huo, lakini pia nawao wanamapungufu ya kwani wao wenyewe pia wanasigana.

Umoja wao sio mkubwa sana kama ilivyo kwa michezo mingine hivyo taa ya kijanai iwawakie ikionesha ishara ya upendo.

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

Leave a Reply

Exit mobile version