Menu
in , , ,

Bayern wawapiga Chelsea Super Cup

Ndoto za kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ‘The Happy One’ zimeota mbawa baada ya kufungwa na Bayern Munich kwenye Super Cup.
Bayern wanaofundishwa na Pep Guardiola walifanikiwa kutwaa kombe hilo kwa mikwaju ya penalty 5-4 baada ya kumaliza dakika 120 kwa kwenda sare ya mabao 2-2.

Bayern wamelipiza kisasi kwa sababu Chelsea waliwafunga nyumbani kwao na kutwaa Kombe la Ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Alikuwa mchezaji kinda aliyetokea kuwa mashuhuri tangu msimu uliopita akiwa kwa mkopo West Bromwich Albion, Romelu Lukaku aliyekosa penati na kupeleka kombe hilo Ujerumani.

Mechi hiyo iliingia kwenye hatua za mikwaju ya penati baada ya bao la Javi Martinez, kwani Chelsea walikuwa mbele kwa mabao 2-1
Chelsea wamecheza mechi hiyo kwa kuwa ni mabingwa wa msimu uliopita wa Kombe la Europa wakati Bayern Munich ndio Mabingwa wa Ulaya.

Wakiongozwa na kocha Pep Guardiola aliyetarajiwa kurejesha uhasimu wake kwa Mourinho, walionekana dhaifu mwanzoni, kwani Chelsea walipata bao la mapema dakika ya saba kupitia kwa Mhispania, Fernando Torres.

Hata hivyo, bao hilo lilisawazishwa katika kipindi cha pili, baada ya Frank Ribery kutungua nyavu dakika mbili tu tangu kuanza kipindi hicho.

Baada ya mechi kulazimika kuingia katika muda wa ziada, Mbelgiji Eden Hazard alifunga bao la pili lililotokea kuwa la ushindi katika dakika ya 93.

Kama ilivyokuwa kwenye mechi dhidi ya Manchester United, Kocha Mourinho alimwanzisha benchi na kumwacha hapo hadi mwisho kiungo mzoefu, Juan Mata na pia nahodha John Terry aliyeingia dimbani dakika ya 113.

Torres ndiye mshambuliaji mpachika mabao pekee aliyeanza mechi hiyo, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Lukaku katika dakika ya 97.
Chelsea walipewa kadi nyingi, moja ikiwa nyekundu aliyozawadiwa Ramires. Nyingine za njano walilambishwa Branislav Ivanovic, Ashley Cole, David Luiz, Gary Cahil, Torres na Lukaku wakati Bayern walipata kadi mbili tu.

Mourinho angetamba kwa kutwaa kombe hilo, wakati Guardiola sasa walau atajidai kwani alikuwa anashutumiwa nchini Ujerumani kwa madai ya kushindwa kuwaongoza vyema Bayern kwenye ligi kuzoa pointi zote.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version