Menu
in , , ,

Bayern waanza usajili

*Wawanasa Hummels, Renato Sanchez

*Arsenal wawanyatia Mahrez na Kante

Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wameanza biashara ya usajili
mapema na pasipo kupoteza muda wamewaliza Manchester United kwa
kusajili mmoja wa wachezaji waliokuwa wakiwafuatilia, naye ni Renato
Sanches wa Benfica.

Bayern ambao wanaondokana na kocha Pep Guardiola anayehamia Manchester
City, kadhalika wamevamia Borussia Dortmund na kumsajili mlinzi Mats
Hummels ambaye nusura ajiunge na Mashetani Wekundu kiangazi
kilichopita.

Hummels, 27, anatarajiwa kujiunga na Bayern kwa mkataba wa miaka
mitano na kilichokuwa kikiendelea sasa ni uchukuaji wa vipimo juu ya
afya yake. Bayern wamewalipa Benfica pauni milioni 27.5 kumpata
Sanches mwenye umri wa miaka 18.

Taarifa zilizopo ni kwamba kocha wa zamani wa Real Madrid, Carlo
Ancelotti atachukua mikoba ya Guardiola hapo Allianz Arena wakati
Guardiola akichukua ya Manuel Pellegrini huku Manchester United wakiwa
bado katika sintofahamu iwapo Louis van Gaal aendelee au wamchukue
JoseMourinho wa zamani wa Chelsea.

Hummels alianzia soka yake Bayern, akacheza mechi moja tu ya
Bundesliga 2007, kabla ya kuhamia Dortmund. Mechi yake ya mwisho
Dortmund itakuwa dhidi ya Bayern katika fainali ya Kombe la Ligi, Mei
21, ikiwa Guardiola atamopanga.

Mtendaji Mkuu wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge anasema kwamba Hummels
ni mmoja wa mabeki wa kati mahiri zaidi duniani na kwamba wakiwa naye,
ni wazi kiwango chao kama timu kitakwenda juu.

Sanches tayari amefanya vipimo vya afya na inaelezwa kwamba naye
amesaini mkataba wa miaka mitano hapo Ujerumani. Bayern wametwaa
ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Rummenigge amemwelezea Renato kuwa
mchezaji anayekwenda na mabadiliko, anashambulia kiakili na kiufundi
na kwamba amejaliwa kipaji kwa asili.

ARSENAL WAWATAKA MAHREZ, KANTE, WALCOTT KUONDOKA?

Could Arsenal’s Theo Walcott be on his way to the Olympic Stadium?
Could Arsenal’s Theo Walcott be on his way to the Olympic Stadium?

Pamoja na kwamba imeelezwa kuwa nyota wa mabingwa wapya wa England,
Leicester, watabaki kwenye kikosi hicho msimu ujao, Arsenal wamefungua
mazungumzo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Riyad Mahrez, 25,
anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 40 na kiungo N’Golo
Kante, 25, anayeweza kuuzwa kwa pauni milioni 20.

Leicester walipanda chati hadi kutwaa ubingwa bila kutarajia, ambapo
baada ya mafanikio hayo kocha Claudio Ranieri angependa kuona nyota
wake wakibaki pamoja kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na mechi za
Ulaya.

West Ham wanasemekana wanaelekeakufanikisha mpango wa kumsajili winga
wa Arsenal na England, Theo Walcott, 27, kwa pauni milioni 20, ili
kujiimarisha kwa msimu ujao, wakimwahidi kumpa nafasi za kuanza mechi
karibu kila mara.

Katika hatua nyingine, mmiliki mwenza wa West Ham, David Sullivan
anasema kwamba wametoa dau la pauni milioni 24 kwa mmoja wa
washambuliaji mahiri zaidi nchini Ufaransa na wasipofanikiwa watatoa
jingine la pauni milioni 25 kwa aliye England.

Inaaminika kwamba anayenunuliwa kwa pauni milioni 24 ni mshambuliaji
wa Marseille, Michy Batshuayi, 22 na dau jingine huenda likaenda
Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji Christian Benteke, 25.

Mshambuliaji wa Atletico, Antoine Griezmann, 25, amewaambia rafiki
zake kwamba yupo tayari kukataa ofa za klabu kubwa za Ligi Kuu ya
England (EPL) ili abaki aliko. Mfaransa huyo amekuwa akifuatwa na
Chelsea, Manchester United na Manchester City.

Nahodha wa Chelsea, John Terry, 35, amesema bado anawapenda klabu hiyo
na angependa kuendelea kucheza soka kwa muda zaidi, lakini inadhaniwa
kwamba anakaribia kusaini mkataba utakaompa pauni milioni 12 kwa mwaka
kwenye Ligi Kuu ya China.

Kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 27, anasubiri kuona iwapo Manchester
United wataanza mazungumzo na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho
kabla ya kuamua iwapo ahamie Old Trafford.

Bosi wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino ana tama ya kumsajili
kiungo wa Liverpool, Adam Lallana, 27, aliyepata kuwa naye klabuni
Southampton, ikisemekana kwamba Spurs watatakiwa kutoa pauni milioni
20.

Mshambuliaji wa kati wa Paris St-Germain, Zlatan Ibrahimovic, 34,
anasema atabainisha hivi karibuni ni wapi atakakocheza msimu ujao,
huku akihusishwa na kujiunga na Manchester United.

Winga Mdachi wa Manchester United, Memphis Depay, 22, ameanza
mazungumzo na kocha wake, Louis van Gaal juu ya hatima yake hapo Old
Trafford, baada ya kuwa na msimu wa hovyo na kulaumiwa na wengi kwa
kuendekeza starehe na vitu vya ghali.

Thierry Henry anatarajiwa kupewa kazi ya kudumu Arsenal, ikidhaniwa
kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Ufaransa atakuwa
kocha wa timu ya vijana ya U-18.

Kiungo wa Spurs, Erik Lamela, 24, anasema angepenad kubaki klabuni
hapo kwa angalau mwaka mmoja zaidi, baada ya kuanza kupewa muda wa
kucheza.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version