Menu
in , , , , ,

AZIZ KI AMEKUWA NI ‘GAME CHANGER’ WA YANGA ..

Kutolewa kwa Yanga katika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika imekuwa ni jambo ambalo linajadiliwa sana kuliko kwa Simba. Kutolewa na klabu ya Mamelodi Sundowns hakujawa jambo kubwa ila  Mjadala mkubwa ni juu ya goli ambalo alifunga mchezaji wa kimataifa toka Burkina Faso  Stephane Aziz Ki alilofunga mnamo dakika ya 58 ambalo lilikataliwa na refa. Goli hilo alilifunga katika mchezo wa marudiano ambao ulifanyika nchini Afrika Kusini. Goli hilo lilikataliwa kwa kigezo cha kwamba mpira haukuingia ndani ya nyavu za goli. Mjadala huo umekuwa mkubwa sana kwani unajadiliwa katika bara zima la Afrika na wadau na wapenzi wa mchezo wa soka. Klabu mbalimbali na maarufu kama vile Raja Casablanca ya Morocco limeiweka katika ukurasa wake wa kijamii na kasha kuanzisha mjadala juu ya lile goli.

Mjadala huo unapelekea hadi baadhi ya wachambuzi kujadili kuhusu uadilifu wa kisoka unaoendelea barani Africa maana kuna baadhi ya wadau wanahisi kwamba bilionea Patrice Motsepe ambaye ndiye anayemiliki klabu ya Mamelodi Sundowns na inawezekana alikuwa na mkono katika kukataliwa kwa goli lile. Bao lile limemtoa hadi naibu waziri wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Hamis Mwinjuma kuishauri klabu ya Yanga kukata rufaa matokeo ya mchezo ule kutokana na kukataliwa kwa goli lile na klabu ya Yanga kupitia kwa wakili wake wameiandikia barua shirikisho la soka barani Afrika kupitia upya maamuzi ya refa aliyoyafanya kwani ni kiashiria ya uwepo wa njama za kupanga matokeo ya mchezo. Kwa watu wenye muono wa mbali wameshaanza kuona kwamba bao lile linawezekana kusababisha Afrika kuanza kutumika kwa teknolojia ya mstari wa goli( goal line technology) katika maamuzi ya mechi za ushindani hususani klabu bingwa barani Afrika.

Tanzania Sports

Aziz Ki hajakuwa tu game changer kwenye mechi hiyo bali amekuwa ni mojawapo ya wachezaji wachache katika ligi kuu ya Tanzania ambao uwepo wao umekuwa unazua mijadala ya hapa na pale baina ya wadau na mashabiki wa soka nchini. Na hata usajili wake ulileta mjadala mkubwa nchini Tanzania. Usajili wa Aziz Ki ulivunja rekodi ya usajili katika klabu ya Yanga ambao hapo awali ulikuwa unashikiliwa na mchezaji kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo aitwaye Djuma Shaban. Inadaiwa alisajiliwa kwa Zaidi ya milioni 200 ambao kwa wakati huo ni kiasi kikubwa cha fedha. Waandishi wa habari walidai kwamba usajili wake ulifanikishwa Zaidi kutokana na ukaribu ambao alikuwa nao na mchezaji mwenzake kutoka nchini Burkina Faso aitwaye Yacouba Sogne. Waandishi wanadai Yacouba ndiye alimwambia ahamie Yanga.

Katika usajili wake Yanga walianzisha mtindo mpya katika soka la Tanzania kwani walimtambulisha Aziz Ki kwenye mitandao ya kijamii na walipost taarifa hizo usiku wa manane na wadau wa soka walikaa mpaka mda huo kwa ajili ya kujua ni mchezaji gani ambaye alikuwa amesajiliwa na Yanga. Hapo awali Yanga walikuwa wametangaza kwamba watatambulisha mchezaji mpya ambaye atatingisha usajili nchini. Mashabiki wakaingia kiu ya kujua ni mchezaji ganio huyo ambaye atakayetingisha usajili nchini kwa hivyo wakakaa mpaka mda huo wa usiku kwa ajili ya kumjua ni mchezaji gani ambaye atatambulishwa.

Baada ya kutambulishwa Aziz Ki klabu ya Yanga chini ya aliyekuwa kocha mkuu wa wakati huo wana Nasreddine Nabi ikaamua kukaa kambi hapa nchini katika kambi ya Avic town Kigamboni badala ya kwenda nje ya nchi wakati wahasimu wao klabu ya Simba walienda nchini Uturuki. Washabiki wa Simba wakaanza kuwatania wenzao wa Yanga kwamba Aziz Ki ameifilisi klabu mpaka wameshindwa kuweka kambi kwa sababu fedha zao zote za kambi zimeishia katika kumsajili Aziz Ki. Usajili wa Aziz Ki ukafungua njia kwa kusajiliwa wachezaji wa daraja la kidunia ambapo tukaona wachezaji kama Gael Bigirimana ambaye aliwahi kuchezea klabu ya Newcastle United ya England na usajili huo ukamsaidia hadi aliyekuwa mjumbe wa kamati ya usajili injinia Hersi Said kushinda uraisi wa klabu ya Yanga bila ya tabu yoyote ile.

Usajili huo ambao ulileta mjadala kwani ilionekana kama Yanga ilitumia pesa nyingi na kama asingeweza kucheza kwa kiwango kikubwa basi pesa ambazo klabu ya Yanga ilizitoa ingekuwa imekula hasara. Katika mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho dhidi ya klabu ya Club Africaine ya nchini Tunisia Aziz Ki ndiye mchezaji aliyefunga goli maridadi ambalo liliisaidia klau yake ya Yanga kuvuka na kwenda kwenye hatua ya robo fainali na kufanya hivyo kukamfanya akawa ni “talk of the town” na kila mtu akawa anamsifia kwamba ni mchezaji muhimu kwani umuhimu wa mchezaji huonekana katika mechi kubwa na nzito. Msimu huu ana Zaidi ya magoli 10 ambayo ameyafunga na inaonyesha mpaka ligi itakapoisha basi kama ataendelea na mwendo huu huu basi inawezekana akawa amefunga magoli mengi Zaidi.

Kuna tetesi za kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinasema klabu za Afrika kusini zinapambana ili kupata saini ya Aziz Ki baada ya kuvutiwa na kiwango ambacho amekuwa anakionyesha katika mechi za hivi karibuni. Miongoni mwa vilabu ambavyo vinatajwa ni pamoja na Mamelodi Sundown, Kaizer Chief na Orlando Pirate. Kwa nguvu kubwa ya uchumi ambayo vilabu hivyo inavyo haitakuwa rahisi kwa timu yake ya Yanga kukataa pesa kutoka kwa matajiri hao wa Afrika kusini.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version