NI muda mrefu sasa tangu taarifa zilipoibuliwa kuwa kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Farid Mussa. Kinda huyo ameibuliwa na Azam akiwa mwenye kipaji cha hali ya juu na kufanikiwa kucheza sambamba na mastaa kama Mbwana Samatta, Nadir Haroub na Thomas Ulimwengu.
Mwishoni mwa mwaka jana iliripotiwa kuwa Farid Mussa hakuidhinishwa kwenye kikosi cha klabu ya Azam kitachoshiriki mashindano ya kimataifa kutokana na kutakiwa kwenda kufanya majaribio nchi za ulaya, zikiwemo Scotaldn na Hispania.
Licha ya taarifa hizo hadi leo hii Farid Mussa bado anaitumikia Azam kwenye mashindano ya Kombe la Mpainduzi yaliyomalizika huko visiwani Zanzibar.
Hata hivyo zipo taarifa zimeibuka kuwa nyota huyo anabaniwa na klabu yake kwenda kwenye kufanya majaribio nje ya nchi.
Azam imedaiwa kuzuia mpango wa kiungo huyo kwenda kucheza soka ya kulipwa Ulaya.
Farid Mussa anatakiwa na klabu za Celtic FC inayoshiriki Ligi Kuu Scotland na Athletic Bilbao ya Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio.
Akizungumza mapema jumatatu jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba alisema mchezaji huyo hauzwi kokote.
Kawemba alisema tetesi za kutakiwa mchezaji wao katika klabu hizo zinavumishwa, lakini hawana mpango wa kumuuza.
Alisema hawafahamu kama wachezaji huyo, anahitajika na klabu nyingine na wanasikia kupitia vyombo vya habari, kwani zimekuwa ni tetesi.
“Farid kwanza hauzwi, tunasikia kupitia katika vyombo vya habari, lakini hatuna ofa yoyote kutoka klabu hizo zinazotajwa,” alisema Kawemba.
Kawemba alisema uongozi klabu hiyo hauwahi kusema katika tovuti yao, lakini sehemu nyingine hata mara moja kuhusu kuuzwa kwa mchezaji wao.
Vita vya Ubingwa yagona Yanga, Azam
USHINDI wa bao 1-0 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es salaam umekoleza mbio za kuwania ubingwa huo msimu huu.
Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi mwishoni mwa wiki baada ya kuinyuka Ndanda FC ya mkoani Mtwara hivyo kuipa kumbo hasimu wake Azam ambayo yenyewe ilitoka sare ya bao 1-1 na African Sports ya Tanga.
Kufuatia ushindi huo Yanga imejikusanyia pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 sawa na klabu ya Azam FC. Yanga imefunga jumla ya mabao 31, imetoka sare mechi 3 na haijafungwa mehzo wowote.
Wakati Azam imetumbukiza wavuni mabao 28, kutoka sare mechi 3 na haikupoteza mchezo wowote. Yanga ilikwea kileleni kutokana na tofauti ya mabao ya kufunga. Zote zimeshinda mechi 11.
JE NANI KUIBUKA MBABE?
Yanga na Azam zimekuwa kwenye mpambano mkali wa kuwania ubingwa msimu huu zikifuatiwa na klabu za Simba ambaye imecheza mechi 14, imeshinda mechi 9, kutoka sare mechi 3 na kufungwa mechi 2, huku ukitumbukiza wavuni mabao 21 na kufungwa mabao 9 na kujikusanyia pointi 30.
Mtibwa Sugar inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 katika mechi 14, ambapo imeshinda mechi 8, kutoka sare 3. Na kufungwa mechi 3. Nafasi ya tano imechukuliwa na Stand United yenye pointi 25 katika mechi 14.
Mkiani zipo timu tatu zinapigana kutoshuka daraja, nazo ni Ndanda Fc yenye pointi 9 katika mechi 14, pamoja na Kagera Sugar yenye pointi 9 katika mechi 14, ikifuatiwa na Africans Sports yenye pointi 8 katika mechi 14.
Mchuano wa ubingwa mwaka huu ni wazi unazihusu Yanga na Azam, lakini tofauti yao na Simba ni pointi 6 ikiwa na maana ya mechi 2 pekee. Kwamba Simba itaombea Yanga na Azam zipoteze mechi zao 2 kila mmoja huku yenyewe ikishinda idadi hiyo ya mechi.
MFUNGAJI BORA
Kinyang’anyiro cha ufungaji bora kinawakutanisha washambuliaji hatari, Amiss Tambwe(Yanga) mwenye mabao 10, akifuatiwa na Hamis Kiiza(Simba) ana mabao 9, Elius Maguli(Stand United) ana mabao 9, na Jeremiah Juma(Prisons) ana mabao 8. Wafungaji hawa wanachuana kuwania tuzo ya mfungaji bora Ligi Kuu Tanzania.