Menu
in , , ,

ARSENE WENGER ATAENDELEA KUWA MNYONGE KWA JURGEN KLOPP?

Tanzania Sports

ARSENE WENGER ATAENDELEA KUWA MNYONGE KWA JURGEN KLOPP?

Mechi nne zimeshawakutanisha ,katika mechi hizi nne Jurgen Klopp
amefanikiwa kushinda mechi tatu na kutoka sare mechi moja na kumfunga
goli 14.

Hii inaonesha ni jinsi gani, Jurgen Klopp amekuwa mtu ambaye ni mbabe
mbele ya Arsene Wenger, na anaingia katika mechi hii akiwa na faida ya
kujiamini zaidi kuliko Arsene Wenger ambaye amekuwa mnyonge sana
kwake.

Kiwango kizuri cha Mesut Ozil kinaweza kikawa silaha nzuri kwa Arsene
Wenger leo ?

Mechi nne zilizopita Mesut Ozil ameonesha kiwango kizuri ambapo katika
mechi dhidi ya Tottenham Hotspurs alifanikiwa kutoa pasi ya mwisho ya
goli.

Mechi dhidi ya Swansea Alitoa pasi moja ya mwisho, huku katika mechi
dhidi ya Huddersfield Town akitoa pasi mbili za magoli na kufunga goli
moja, na mechi dhidi ya Newcastle akifunga goli moja.

Hii inaonesha kwa sasa Mesut Ozil ndiye mchezaji bora katika kikosi
cha Arsenal kwani upikaji na upatikanaji wa magoli kimekuwa kitu
amɓacho kinawasaidia sana Arsenal.

Oxlaide Chamberlaine kurejea kwake kwa mara ya kwanza pale Emirates
kutakuwa na faida au hasara kwa Liverpool?

Kakaa zaidi ya miaka mitano pale Arsenal , kwake pale ni kama
nyumbani, anarudi tena kwa mara ya pili, mapokeo ya kurudi kwake
ndicho kitu ambacho kitazalisha matokeo hasi au chanya kwa Liverpool.

Kama Oxlaide Chamberlain atakuwa amechukulia jambo lake la kurudi
katika hali ya kupania sana kutakuwa hakuna madhara sana, kwani
atataka kuonesha kama anataka kuiadhibu timu yake ya zamani, hivo
atakuwa anakosa umakini kwenye maamuzi yake.

Lakini akiipokea kawaida hali ya kurudi kwake Emirates akiwa na jezi
nyingine kutakuwa na msaada mkubwa kwa Liverpool kwa sababu atakuwa na
nafasi kubwa ya yeye kukaa na kufanya maamuzi kwa utulivu ,maamuzi
ambayo yatakuwa na msaada kwake na timu kwa ujumla.

Hali ya uwanja wa Emirates utakuwa na msaada mkubwa kwa Arsenal?

Hapana shaka Arsenal amekuwa na matokeo mazuri katika uwanja wake wa
nyumbani, kwani amefanikiwa kutopoteza mechi 13 kati ya mechi 14
ambazo amecheza pale, hii inaonesha ni jinsi gani ambavyo Arsenal
amekuwa akitumia vizuri uwanja wake wa nyumbani na Liverpool
wasitegemee mchezo mwepesi.

Kurejea kwa Philipe Countinho kutakuwa na msaada gani katika kikosi
cha Liverpool ??

Moja ya wachezaji ambao wana historia nzuri na Arsenal ni Philippe
Countinho, hivo kurejea kwake kutakuwa na faida kubwa sana Liverpool.

Liverpool watakuwa wamepata kiungo amɓaye ana uwezo mkubwa wa
kutengeneza nafasi nyingi za magoli, hivo kutawapa nafasi kina
Mohammed Salah, Saido Mane, na Firmino kuchezeshwa kwa kiasi kikubwa.

Ubovu wa beki ya Liverpool utakuwa na faida kwa Arsenal?

Pamoja na kwamba Liverpool ina safu hatari ya kushambulia lakini safu
yake ya ulinzi haijaimarika sana hasa hasa kwenye mashambulizi ya
kushtukiza.

Liverpool mbele imekuwa na wachezaji wenye kasi tofauti na nyuma
ambapo wamekuwa na wachezaji ambao hawana kasi sana, hivo kupelekea
kutohimili vizuri mashambulizi ya kushtukiza, na pia beki yao imekuwa
na makosa mengi binafsi.

Aaron Ramsey kutakuwa na faida kwa Liverpool?

Katika mechi ya mwisho kukutana kwa hizi timu ambapo Liverpool
ilishinda goli 4, mchezaji pekee ambaye alionekana na uhai katika
kikosi cha Arsenal alikuwa Aaron Ramsey.

Leo hayupo, itakuwa ni pigo kubwa sana katika kikosi cha Arsenal kwa
sababu ndiye mchezaji pekee aliyekuwa analeta uwiano mzuri katika eneo
la kujilinda na eneo la kushambulia kwa kutumia uwezo wake wa kukimbia
kutoka eneo lake mpaka eneo la mpinzani.

Matokeo mabovu dhidi ya timu kubwa msimu huu itakuwa moja ya sababu
kwa Liverpool kupoteza mechi hii??

Msimu huu wamecheza mechi tano dhidi ya timu kubwa na kupata alama 5
tu, hii ni tofauti na msimu jana ambapo walipata alama nyingi dhidi ya
timu kubwa.

Hii imepunguza kwao kujiamini wanapokutana na timu kubwa tofauti na
msimu jana , hii ikichukuliwa katika mlango chanya inaweza ikawa faida
kubwa sana kwa Arsenal kwenye mechi hii.

mail to: martinkiyumbi@gmail.com

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version