Menu
in , , ,

Arsenal wawanyonga Man U 3 – 0

Arsenal wamewashangaza Manchester United kwa kuwacharaza 3-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Washika Bunduki wa London walifunga mabao hayo katika dakika 20 za mwanzo wa kipindi cha kwanza, na ushindi huo kuwapandisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

United wanaofundishwa na kocha Louis van Gaal aliyekuwa ameanza kupata mafanikio Old Trafford hakupata jibu dhidi ya Arsenal ambao walifungua mauaji yao kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil kufunga mabao ndani ya sekunde 74 tu.

Sanchez aliongeza bao la tatu akifunga kutoka umbali wa yadi 18, hii ikiwa ni mara ya pili tu kwa Arsenalkupata ushindi dhidi ya United katika mechi 14 zilizopita. Ni mara ya pili Arsene Wenger kumfunga Van Gaal, Arsenal wakiwa pia wamefungwa mara moja na kwenda sare mara moja.

http://www.youtube.com/watch?v=CUc34cThFb8

Mashetani Wekundi walijiimarisha baada ya nusu saa lakini hawakuweza kuipita ngome ya Arsenal na nusura wafungwe bao la nne  lakini mpira wa Alex Oxlade-Chamberlain uligonga mwamba. Kichapo hiki kinawaacha Man U kwenye nafasi ya tatu, wakiwa wamezidiwa na Arsenal na uwiano wa mabao.

Katika mechi nyingine Jumapili hii, Everton wamekwenda sare na Liverpool kwa kufungana bao 1-1 wakati Swansea na Totttenham Hostpur nao wametoshana nguvu kwa kufungana 2-2.

Ozil, alikuwa na siku njema uwanjani.
Ozil, alikuwa na siku njema uwanjani.

Wakati bao la Liverpol lilifungwa na Dany Ings dakika ya 11, la Everton lilitiwa kimiani na Romelu Lukaku dakika ya 45.

Mabao ya Swansea yalifungwa na Andre Ayew na bao la kujifunga la Harry Kane wakati Spurs wakifunga kupitia kwa Christian Eriksen.

Jumamosi Manchester City waliwafyatua Newcastle 6-1, Crystal Palce wakawakanyaga West Bromwich Albion 2-0, Bournemouth wakaenda sare ya 1-1 na Watford, Norwich wakalala 1-2 kwa Leicester, Sunderland wakaenda sare ya 2-2 na West Ham na Chelsea wakalala 1-3 kwa Southampton hapo Stamford Bridge.

Kwa matokeo hayo sasa Manchester City wapo kwenye uongozi wa ligi wakiwa na pointi 18, wakifuatiwa na Arsenal na Man U wenye pointi 16. Wanafuatiwa na Crystal Palace na Leicester wakiwa na pointi 15.

Aston Villa wenye pointi nne wapo na Sunderland na Newcastle wenye pointi tatu.

Advertisement

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version