Arsenal wamefanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuwafunga Aston Villa 2-1.
Ilikuwa faraja kwa Arsene Wenger kuwageuzia kibao wale waliowaadhiri mwanzoni mwa msimu kwa kuwakung’uta 3-1.
Kiungo Jack Wilshere aliendelea kuonesha tambo zake badada ya kufunga dakika ya 34 na mshambuliaji tegemeo, Olivier Giroud akagunga dakika moja tu baadaye.
Villa walipata bao la kufutia macozi dakika ya 76 kupitia kwa Christian Benteke ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia katika moja ya klabu kubwa za EPL.
Kwa matokeo hayo Arsenal wamewavuka Manchester City walioshikilia usukani kwa siku moja tu.
Villa walipoteana muda mwingi, wakionekana kama watu wanaopoteza vivuli na kuwawekea Washika Bunduki wa London rekodi ya kutofungwa Villa Park kwa mechi 15 tangu Desemba 1998.
Gunners walifurahishwa na kurejea dimbani kwa Alex Oxlade-Chamberlain aliyecheza dakika chache za mwisho wa mchezo, hasa wakati huu ambapo Theo Walcott ameumia na majaliwa ni kwamba hatacheza tena hadi mwisho wa msimu.
Kwa matokeo hayo na mengine ya mwisho wa wiki, Arsenal wanaongoza ligi wakiwa na pointi 48 wakifuatiwa na Man City na Chelsea ambapo kila timu inapungukiwa pointi moja.
Baada ya timu zote kucheza mechi 21, wanaofuatiwa katika nafasi ya nne ni Liverpool, Everton, Tittenham Hotspur wakati Manchester United bado ‘wamepindenda’ nafasi ya saba.
Wengine kwa kushuka katika nafasi yao ni Newcastle walio ya nane wakifuatiwa na Southampton, Hull, Villa, Stoke, Swansea, West Bromwich Albion, Norwich, Fulham na West Ham.
Walio katika lile dimbwi la kushka daraja ambao ni Cardiff, Sunderland na Crystal Palace ambazo zimeshatengewa mahitaji muhimu.