Menu
in , , ,

Arsenal Vs Chelsea: Ngao ya Hisani..

Tanzania Sports

Mwaka 2005 na mwaka 2015 ni miaka ambayo timu hizi zilikutana kwenye
mechi ya ngao ya hisani.

Chelsea akishinda mwaka 2005 na Arsenal akishinda mwaka 2015. Hii yote
inaonesha kuwa mechi hii ya leo itakuwa na nafasi kubwa ya kumuonesha
ni nani ambaye ni mbabe kati ya Arsenal na Chelsea kwenye mechi za
ngao ya hisani.

Kutokuwepo kwa Bakayoyo kutakuwa na madhara kwa Chelsea na faida kwa Arsenal ?

Bakayoyo ni majeruhi lakini hivo atakosa mechi ya leo, kukosa kwake
katika mechi ya leo kutakuwa na faida kubwa sana kwa Chelsea na hasara
kwa Arsenal.

Bakayoyo ni mchezaji mpya kwenye kikosi cha Conte hivo mpaka sasa
hajaingia kwenye umbo la timu hivo ingekuwa ngumu kwake kuzoea kwenye
kikosi kwa haraka ukizingatia mechi hii ni kubwa sana.

Sasa faida watakayopata Chelsea ni ipi ?

Chelsea itakuwa na nafasi ya kumwanzisha Kante pamoja na Fabregas
katika eneo la kati. Kante atakuwa huru katika eneo la chini kwa
kuwalinda mabeki wake kitu ambacho kitamsaidia Fabregas kucheza juu,
kucheza eneo la juu kwa Fabregas kutampa nafasi kubwa yeye kuwa na
wastani mzuri wa kutengeneza nafasi kwa pasi zake za mwisho. Fabregas
ni moja ya wachezaji ambao wanauwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za
magoli, hivo kumchezesha na Kante ambaye pamoja na kuwa ni mzuri kwa
kuzuia pia ni mzuri kwa kuanzisha mashambulizi hivo kumpa nafasi kubwa
Fabregas kutengeneza nafasi za magoli pamoja na kufunga.

Victor Moses pamoja na Laurent Koscienly watakuwa na nafasi ya kuanza
leo baada ya kufutiwa adhabu yao ya kadi nyekundu.

Hii itakuwa na faida kubwa kwa Chelsea kuliko Arsenal, kwanini nasema hivo ?

Funguo ya mashambulizi ya pembeni huwa yanakuwa na uhai mkubwa kwenye
upande anaocheza Moses.

Kutokuwepo kwa Moses kungeleta kutokuwa na presha kubwa eneo la upande
wa kulia , uwepo wake unafanya presha hiyo ibaki kuwepo na Chelsea
kuwa na uhakika mkubwa wa kutengeneza nafasi nyingi kupitia eneo la
kulia. Pia Moses analeta uwiano mzuri kati ya eneo la kuzuia na
kushambulia.

Hata mechi ya fainali ya FA CUP, Arsenal walipata nguvu baada ya Moses kuumia.

Sanchez atakuwa na nafasi kubwa ya kuibeba Arsenal?

Hakuwa na timu kwenye mechi za kujiandaa na Msimu, hii haipotezi maana
ya kwamba yeye ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal.

Uwepo wake katika eneo la mbele utamfanya acheze kama mchezaji huru
katika eneo la mbele akiwa nyuma ya Lacazatte au Giroud. Uwepo wake
katika eneo hili huru utamfanya aweze kutengeneza nafasi nyingi za
kufunga pamoja na kufunga goli. Na hii itawapa uhai Lacazatte au
Giroud kung’ara.

Wakati Arsenal wakiwa na Sanchez kikosini, Chelsea wanaenda kumkosa
Hazard ambaye ni mtu pekee ambaye ubunifu wote wa mbele huanzia kwake.
Hivo hii itampa nafasi ya Willian kuanza.

Kuanza kwa Willian katika eneo la Hazard kutakuwa na faida na hasara
zake, faida ni kwamba kasi, ubunifu na ufungaji wa magoli wa Willian
utakuwa na faida kubwa kwenye timu ila hasara ni kwamba Willian mara
nyingi hurudi chini kusaidia kukaba hivo kutawafanya viungo wa kati wa
Arsenal kusogea mbele kusaidia kusogeza mashambulizi mbele.

Martin Kiyumbi

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Exit mobile version