*Watolewa UCL, kumkosa Ozil
Arsenal wametolewa kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na pia watamkosa kiungo wao mahiri wa Kijerumani, Mesut Ozil aliyeumia.
Arsenal walitolewa rasmi kwenye mashindano nchini Ujerumani walikorudiana na Bayern Munich na kwenda sare ya 1-1 baada ya Bayer kuwafunga Arsenal 2-0 dimbani Emirates wiki tatu zilizopita.
Ozil (25) anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kubanwa na misuli ya nyuma ya mguu juu ya goti na alitarajiwa kuchunguzwa zaidi na matabibu.
Arsenal sasa watawakosa viungo wawili wa kimataifa, Ozil na Jack Wilshere lakini habari njema ni kwamba Aaron Ramsey anarejea uwanjani na pia mchezaji mpya, Kim Kallstrom anaweza kuanza kucheza mechi ijayo baada ya kuwa ameumia mgongo mazoezini Januari hii.
Ramsey ndiye mchezaji bora wa Arsenal kwa msimu huu na aliwasaidia kupachika mabao tangu mwanzo wa msimu huu kabla ya kuumia na inasemekana katika mkataa wake mpya anaongezwa mshahara mara dufu.
Arsenal wamepoteza mechi hizo kwa uwiano wa mabao 3-1 ambapo Bayern walipata penati usiku wa Jumatano kama walivyopata Emirates.
Ilitokana na mchezaji yule yule, Arjen Robben na kama ilivyowakuta kwenye mechi ya kwanza, Bayern walipoteza penati yao na pia Kocha Arsene Wenger alilalamika kwamba haikuwa sahihi kutolewa penati baada ya Laurent Konscielny kuonekana kumchezea vibaya Robben.
Wenger amesema haikuwa haki na kwamba sababu ya Arsenal kutolewa mashindanoni ni kadi nyekundu iliyotolewa kwenye Emirates kwa kipa wao, Wojciech Szczensny kwa madai ya rafu mbaya dhidi ya Robben. Jumatano hii kipa Lukasz Fabanski aliokoa penati ya Bayern.
Bayern wanatafuta njia za kuwa timu ya kwanza katika historia ya UCL kutetea ubingwa. Walitwaa ubingwa huu mwaka jana baada ya kuwachapa wapinzani wao kwenye Bundesliga, Borussia Dortmund katika fainali.
Katika mechi nyingine ya 16 bora Jumanne hii, Atlético Madrid waliwafyatua AC Milan 4-1 na kuwafungisha virago kwa jumla ya mabao 5-1. Mabao ya Madrid ya Jumanne hii yalifungwa na
Diego Costa mawili, Turan na Raúl García wakati
Kaká alifunga la kufutia machozi kwa Wataliano.