Menu
in , , ,

Arsenal kumsajili Yepes?

Arsenal wanafikiria kumsajili beki wa kati, Mario Yepes kuziba pengo la nahodha wao wa zamani waliyemuuza Barcelona, Thomas Vermaelen.

Habari hizi zimekuja kwa mshituko masikioni mwa washabiki wa Arsenal, kwa sababu Yepes ana umri wa miaka 38 na klabu hii imekuwa na kawaida ya kuwa na wachezaji vijana na wakishafika umri wa miaka 30 huongezwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja tu.

Ni suala la umri lililowafanya kusita kumwongeza mkataba Bacary Sagna, lakini Manchester City waliposema wanamtaka, ndipo nao wakataka kumwongezea mwaka mmoja, kisha wakampa mitatu lakini wakawa wamechelewa.
Arsene Wenger, katika siku ya mwisho ya usajili alikuwa Roma, Italia akichezesha mechi ya hisani lakini alifanikisha usajili wa mshambuliaji, Danny Welbeck kutoka Manchester United bali akashindwa kumpata mlinzi Matija Nastatic wa Man City.

Yepes ni mchezaji mzuri na amekuwa kwenye Timu ya Taifa ya Colombia, ambapo angeweza kuungana vyema na kipa mpya wa Arsenal kutoka Colombia, David Ospina. Klabu zinaruhusiwa kuendelea na usajili sasa, lakini kwa wachezai huru tu, kwani dirisha la wenye mkataba limeshafungwa.

Arsenal wanataka kupata ufumbuzi wa muda mfupi, hadi walau Januari watakapojaribu kupata mlinzi mahiri wa kati. Yepes amechezea AC Milan, Paris Saint-Germain na baadaye Atalanta.

Yepes alicheza mechi nne kati ya tano za fainali za Kombe la Dunia, na alikuwa fiti kwa dakika zote 90 za kila mechi. Tatizo lililopo kwa Arsenal ni iwapo majeruhi wataendelea kwaandama kwenye beki ya kati.

Wanawatarajia zaidi Per Mertesacker, Laurent Koscielny, Calum Chambers, lakini pia wanaweza kumtumia kijana Mwingereza Isaac Hayden (19) ambaye ameonesha matumaini makubwa kwenye beki ya kati, lakini anakosa uzoefu wa mechi kubwa na za kimataifa.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version