Menu
in , , ,

Arsenal fainali FA

*Everton nafasi ya nne EPL

Arsenal wamefanikiwa kufika fainali ya Kombe la FA baada ya kuwavua ubingwa Wigan Athletic waliopambana hadi dakika ya mwisho.
Vijana hao wa Arsene Wenger wamemaliza miaka minane bila ya kuwa na taji lolote ambapo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya England pia wametokea kuwa na tatizo kubwa la majeruhi.
Wenger alikuwa amesema wangetumia nguvu zote kuhakikisha kwamba wanasonga mbele kwenye hatua hii ngumu dhidi ya Wigan ambao waliwafyatua Manchester City kwenye fainali mwaka jana.
Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Wembley Wigan walioanza kuonesha ukali wao pale Jordi Gomez alipofunga kwa bao la penati lakini Mkuu wa Nidhamu wa Arsenal, Per Mertesacker alifunga dakika za mwisho na kuweka hai ndoto za Arsenal kupata taji lolote msimu huu.
Kipa wa Arsenal aliyeamua kuhama baada ya msimu huu, Lukasz Fabianski aliokoa penati ya kwanza ya Wigan na kuwapa nguvu Arsenal, ambapo wapogaji wa Arsenal, Mikel Arteta, Kim Kallstrom na Olivier Giroud walifunga penati zao huku James McArthur na Jean Beausejour wakifunga kwa upande wa Wigan, akabaki Santi Cazorla aliyewavusha Gunners kwenye fainali hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

LIGI KUU EVERTON WAWAPITA ARSENAL

Katika mechi ya Ligi Kuu ya England Everton waliowafunga Arsenal 3-0 majuzi wamewavuka baada ya kuwafunga Sunderland 1-0 na kufikisha pointi 66 wakati Arsenal wanazo 64.
Everton walipata bao lao pekee kupitia kwa mchezaji wa Sunderland, Wes Brown aliyejifunga kwa bahati mbaya katika dakika ya 75 wakati ambapo muda wote kabla na baada Sunderland waligangamala.
Kwenye mechi nyingine Jumamosi hii Crystal Palace wanaotamba sasa na kocha Tony Pulis waliwapiga Aston Villa 1-0, Fulham wakawanawisha Norwich idadi hiyo hiyo ya bao na Southampton wakaangukia kwa Cardiff kwa 0-1 wakati Stoke wakiwachekecha Newcastle 1-0 na West Bromwich Albion wakienda 3-3 na Tottenham Hotspur.
Timu nne za juu kwa mtiririko ni Liverpool, Chelsea, Manchester City, Everton na Arsenal wakati za chini kabisa ni Sunderland, Cardiff na Fulham.
Jumapili hii kuna mechi muhimu abapo Liverpool watawakaribisha Manchester City wakati Chelsea watakaribishwa huko Wales kupambana na Swansea.

-6.77263639.220179

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version