Menu
in , , ,

Argentina wawazidi Ubelgiji

Argentina wamefanikiwa kulinda hadhi yao kwa kuwashinda chipukizi Ubelgiji kwenye mechi ya robo fainali.
Argentina walifanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia kupitia bao la dakika ya nane la Gonzalo Higuain.

Mshambuliaji huyo wa Napoli alifunga kutokana na makosa ya mabeki wa Ubelgiji kutojipanga vyema wakati huo chini ya nahodha Vincent Kompany.
Higuain aliyetoka Real Madrid kwenda Napoli, alifunga baada ya mpira wa Angel Di Maria kugonga mtu, akauingiza kirahisi langoni.

Ubelgiji walishindwa kuunganisha vyema pasi wakati wa kuondoa mpira langoni mwao, ukawakuta adui walioingia kwa kasi kabla ya kujikuta wakikubali bao.
Argentina walicheza na nyota wao Lionel Messi aliyetamba kidogo na pia kubanwa nyakati nyingi na Wabelgiji huku Angel Di Maria wa Real Madrid akilazimika kutoka kipindi cha kwanza baada ya kuumia paja.

Ubelgiji walishituka baadaye na kuanza kushambulia lakini hawakufanikiwa kuziona nyavu, kwa kukosa shabaha au mabeki wa Argentina kuokoa.
Kadhalika nyakati za mwisho Ubelgiji walicheza kwa nguvu na hasira kiasi cha kujivuruga kwa kuotea au kujikuta wakicheza rafu zisizo na sababu.
Divoc Origi mwenye asili ya Kenya ndiye aliyeanza kama mshambuliaji wa kati lakini hakuchanua na Romelo Lukaku alipoingia baada ya saa nzima alitia kashikashi lango la Argentina.

Mchezaji wa Manchester United, Marouane Fellaini aliwatisa Argentina dakika za mwisho kwa kupelekewa mipira ya juu lakini pia alishindwa kujiweka sawa kuimalizia.
Messi amefikia rekodi ya Diego Maradona kwa kulichezea taifa lake mechi 91, na anatarajiwa kuivunja kwa vile bado ana mechi mbele yake na umri bado ni mdogo.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version